Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / DC KATAMBI ATINGA MTAANI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA

DC KATAMBI ATINGA MTAANI KUPAMBANA NA MADAWA YA KULEVYA

guuu-660x400

Na.Alex Sonna,Dodoma

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Patrobas Katambi, amefanya operation ya kushtukiza katika maeneo ya katikati ya Jiji la Dodoma  na kuwa baini vijana wanaotumia madawa ya kulevya aina ya gundi tatizo ambalo limekuwa sugu katika Jiji la Dodoma.

Katika operation hiyo Katambi amefanikiwa kuwakamata vijana ambao wamekuwa wakitumia madawa hayo ambayo yamekuwa yakiwaathiri vijana kwa kiasi kikubwa kwani gundi hiyo wakivuta imekuwa ikiwalewesha.

Hata hivyo waathirika wa madawa hayo wamemuonesha mahali ambapo wamekuwa wakinunua madawa hayo, na Mkuu wa Wilaya kuweka mtego wa kuwanasa wauzaji hao, kwa kuwatuma watumiaji hao na kufanikiwa kumkamata muuzaji wa duka hilo Veronica Valerian, pamoja na mmiliki wa duka hilo Hechikael Valerian.

Hata hivyo Mmiliki wa duka hilo aliwakana vijana hao kwa kudai kuwa hawafahamu wala hajawahihi kuwauzia gundi, mara baada ya kufikishwa katika kituo cha cha polisi kati Dodoma, wauzaji walikili kuwauzia watoto hao, lakini wakidai mmiliki wa duka alikuwa hatambui biashara hiyo.

“Ni kweli tunawauzia gundi lakini mama hatambui ndio maana alikataa kutambua biashara hiyo na alikuwa hatambui chochote kuhusu swala hili na hakuona biashara hiyo.” Alisema Veronica

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Patrobas Katambi amesema ameamua kufanya operation hiyo baada ya kuona vijana wadogo wanateketea katika janga hilo la uvutaji gundi ambalo limekuwa likiathiri watoto wengi hapa mjini.

“ Nimeamua kufanya operation hii kwa sababu nimeona vijana wengi hapa mjini wanateketea katika janga  hili na tusipo chukua hatua watoto wetu wataharika zaidi, sababu janga limekuwa kubwa.” Alisema Katambi.

Amesema na vijana wengi walioingia kwenye janga hili si wakazi wa Dodoma, bali ni wale waliotoka nje ya Dodoma, waliokuja kutafuta maisha lakini kutokana na umri wao kuwa mdogo wanakosa fursa hali inayowapelekea kuingia katika janga la uvutaji wa madawa ya kulevya.

Amesema vijana hawa hununua gundi na kuiweka kwenye vikopo na kuanza kuivuta hali inayopelekea vijana hawa kulewa, na ukivuta gundi hii inapelekea kuhalibu mfumo wa fahamu na kupoteza uwezo wa kufikili na kupelekea  kuhalibika na kuwa vibaka mitaani.

Vilevile amezitaka jamii kulichukulia kwa uzito swala hili kwa sababu ni kinyume na maadili yetu  na kinyume na sheria za Nchi yetu kwahiyo kila mtu anawajibu wa kuzuia vitendo hivi.

 

About Alex

Check Also

AA

WASICHANA WATATU NA MMOJA KATI YA WAVULANA SABA WAFANYIWA UKATILI WA KINGONO KABLA YA MIAKA 18

Takwimu za vitendo vya ukatili kwa watoto nchini  vinaonyesha kuwa mmoja kati ya wasichana watatu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 − 10 =