Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / MANYARA YATEKELEZA KAMPENI YA VIWANDA 100 KILA MKOA

MANYARA YATEKELEZA KAMPENI YA VIWANDA 100 KILA MKOA

IMG-20181114-WA0104
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akisalimiana na wananchi wa Mkoa wa Manyara, alipowasili leo Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro kwenye ziara yake ya kutembelea wilaya za Simanjiro, Babati na Hanang. 
IMG-20181114-WA0105
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa huo kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan. 
………………….
MKOA wa Manyara umetekeleza kampeni ya kuanzisha viwanda 100 kwa kila mkoa yenye kauli mbiu ya ‘mkoa wangu kiwanda changu’ kwa kuweka mikakati ya kila halmashauri ya Wilaya kuanzisha viwanda 15. 
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti aliyasema hayo wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya mkoa huo kwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan alipowasili mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro kwenye ziara ya kizazi. 
Alisema hadi Septemba 30 mwaka huu mkoa una viwanda vipya 29 vinavyofanya kazi, viwanda 25 vimekarabatiwa na vinafanya kazi, viwanda tisa ujenzi unaendelea na sita ujenzi haujaanza. 
Alisema wana matarajio kuwa Manyara itafikia malengo yake ya viwanda vipya 100 kabla ya Desemba mwaka huu. 
Alisema mkoa huo unaendelea kuhamasisha wananchi wake kuwekeza kwenye sekta ya viwanda ili kukuza hali ya uchumi ya mkoa na Taifa kwa ujumla, kutoka uchumi wa chini kwenda wa kati. 
Alisema mkoa una viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ambazo vimegawanyika katika makundi manne. 
Alisema kundi la kwanza ni viwanda vidogo sana, kundi la pili ni viwanda vidogo, kundi la tatu ni viwanda vya kati na kundi la nne ni viwanda vikubwa. 
“Kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2013 za ofisi ya takwimu ya Taifa zinaonyesha kuwa mkoa wa Manyara una viwanda 2,400 kati ya hivyo viwanda vidogo sana ni 2,067 vidogo 305, vya kati 14 na vikubwa ni 14,” alisema Mnyeti. 
Alisema mkoa kwa kushirikiana na Sido ulifanya mkutano wa kuzindua mkakati wa uanzishaji wa viwanda kwa mfumo wa kongamano Mei 31 mwaka 2017.
Akizungumza baada ya kupokea taarifa hiyo Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan aliipongeza Manyara kwa kupiga hatua kwenye sekta mbalimbali. 
Hata hivyo alisema bado juhudi zinahitajika kwa upande wa lishe kwani mkoa huo unazalisha chakula kingi lakini kuna tatizo la lishe kwa watoto. 

About Alex

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × two =