Monday , February 18 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA TAKUKURU KATIKA KIPINDI CHA JULAI, 2018 HADI SEPTEMBA, 2018 MKOA WA TABORA

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UTEKELEZAJI WA MAJUKUMU YA TAKUKURU KATIKA KIPINDI CHA JULAI, 2018 HADI SEPTEMBA, 2018 MKOA WA TABORA

index

TAKUKURU Mkoa wa Tabora imeendelea kutekeleza majukumu yake ya Kuzuia, Kupambana na kuelimisha jamii katika mapambano dhidi ya Rushwa huku ikitekeleza majukumu hayo kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na Rushwa namba 11/2007. TAKUKURU imegawanya shughuli zake katika sehemu kuu tatu ambazo ni Uchunguzi, Elimu kwa Umma pamoja na Udhibiti/ Utafiti.

 • UCHUNGUZI

Kazi zilizofanyika kwa kipindi cha Julai, 2018 hadi Septemba, 2018

 • Jumla ya malalamiko yalipokelewa na kufunguliwa majalada ni 24
 • Majalada yaliyokamilika na kuwasilishwa kwa Mkurugenzi Mkuu ni 7.
 • Kesi mpya zilizofunguliwa mahakamani ni 6.
 • Kesi zilizoisha mahakamani ni 1 ambapo Jamhuri Imeshinda

 • ELIMU KWA UMMA

Kazi zilizofanyika kwa kipindi cha Julai, 2018 hadi Septemba, 2018

 • Semina kwa watumishi katika idara mbalimbali za umma na sekta binafsi ni 43
 • Mikutano ya hadhara 33 ilifanyika katika vijiji na kata
 • Ufunguzi/Uimarishaji wa vilabu vya wapinga Rushwa katika shule za msingi,sekondari na vyuo  ni 136
 • Vipindi vya redio 8 vilirushwa  kupitia uhai Fm.
 • Onesho moja(1) lilifanyika katika viwanja vya nanenane Ipuli .

 • UDHIBITI

Katika kipindi cha Julai, 2018 hadi Septemba, 2018, TAKUKURU (M) Tabora ilitekeleza majukumu yake kama ifuatavyo

 • UDHIBITI/UCHAMBUZI WA MIFUMO YA UTENDAJI

Uchambuzi wa mifumo mitano(5) ya idara na taasisi za umma/binafsi ilichambuliwa ili kubaini upungufu/mianya ya Rushwa iliyopo.

 • WARSHA NA VIKAO VYA WADAU

Warsha na vikao vya wadau viwili (2) vilifanyika kujadili matokeo ya uchambuzi wa mfumo ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ya kuziba mianya ya Rushwa iliyobainika.

 • TAARIFA ZA UTEKELEZAJI

Taarifa za utekelezaji wa maazimio katika vikao vya wadau 2 zilitolewa

 • MIRADI YA MAENDELEO

Miradi ya maendeleo katika idara za maji, afya, ujenzi, kilimo/umwagiliaji na elimu imeendelea kufuatiliwa kwa lengo la kudhibiti ubora kwa thamani ya fedha zilizotolewa na kutumika. Ikumbukwe kwamba katika zoezi hili la ufuatiliaji wa miradi tunapobaini kasoro au upungufu tunatoa maelekezo ya kurekebisha kasoro hizo au kurejeshwa fedha na endapo tukibaini kuwepo kwa ubadhirifu katika mradi tunaanzisha uchunguzi wa kina.

 • FEDHA ZILIZOOKOLEWA

TAKUKURU imeokoa  jumla ya shilingi 6,202,500 zilizorejeshwa hazina kupitia akaunti ya Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU iliyoko Benki Kuu.Fedha hizi zilitokana na malipo hewa/ubadhirifu na ukiukwaji wa taratibu za malipo katika sekta ya afya.

6.0     HITIMISHO

Natoa wito kwa jamii kuendelea kutoa ushirikiano kwetu na kushiriki kikamilifu katika mapambano dhidi ya Rushwa, kwa kuzingatia kuwa mapambano dhidi ya Rushwa ni jukumu la kila mwananchi na tukifanya hivyo tutakuwa tunaunga mkono jitihada za viongozi wetu wa kitaifa ambao wamekuwa mstari wa mbele katika mapambano dhidi ya Rushwa na ufisadi.

           Daima kauli mbiu yetu  iwe “Kataa Rushwa,  Penda nchi yako“

Imetolewa na,

 1. MOGASA

MKUU WA TAKUKURU MKOA

15, Novemba, 2018

About Alex

Check Also

hqdefault

ALIYOYASEMA KAIMU MSAJILI WA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI NCHINI BI. NEEMA MWANGA BAADA YA KUTEMBELEA BAADHI YA MASHIRIKA YALIYOPO MKOANI KILIMANJARO

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nine + three =