Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / TUMEAMUA KOROSHO YOTE IBANGULIWE NCHINI-MHE HASUNGA

TUMEAMUA KOROSHO YOTE IBANGULIWE NCHINI-MHE HASUNGA

 

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akieleza malengo ya ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho jana tarehe 13 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga akizungumza na waandishi wa habari kuelezea malengo ya ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho jana tarehe 13 Novemba 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-Wizara ya Kilimo)

 

Na Mathias

Canal-Wizara ya kilimo, Mtwara

 

Waziri wa kilimo Mhe Japhet Hasunga amesema kuwa wizara yake

itatekeleza maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John

Pombe Magufuli kuhakikisha kuwa korosho yote inabanguliwa hapa nchini.

 

Ameyasema hayo jana tarehe 13 Novemba 2018 wakati akieleza malengo ya

ziara yake mkoani Mtwara na Lindi alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari

katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara kabla ya kuanza kukagua

maghala ya kuhifadhia korosho.

 

Hasunga alisema kuwa kuruhusu wafanyabiashara kubangulia nje ya nchi korosho

za wakulima wa Tanzania ajira nyingi zilikuwa zikipotea huku watanzania

wakisalia kuhangaika kutafuta ajira kwani ajira nyingi zilipelekwa nje ya nchi.

 

“Baada ya kujiridhisha tumeamua sasa hahutasafirisha korosho ghafi tunataka

korosho yote iwe inachakatwa nchini kwenye viwanda vyetu, kwa hiyo korosho zote

zilizokuwa zinachukuliwa na wafanyabiashara kwenda kubanguliwa sijui wapi huko

tumezuia” Alikaririwa Mhe Hasunga

 

Alisema kuwa viwanda vya kubangua korosho nchini vingi vimekufa kwa

sababu ya ubadhilifu wa wananchi wachache na baadhi ya hujuma za watu lakini serikali

imedhamiria kuanza kubangua kwenye viwanda vilivyopo kabla ya hatua za

kuanzisha viwanda vingi vya ubanguaji.

 

“Tunamuwezesha

mkulima kwa bei ya shilingi 3300 ili imsaidie kufanya kazi zake zingine ili

aweze kuongeza uzalishaji katika msimu ujao wa mwaka 2018/2019 na kuepuka

kushuka kwa uzalishaji” Alisisitiza Mhe Hasunga

 

Alisema

baada ya kukamilika uhakiki wa maghala yote ya kuhifadhia korosho serikali

itaanza kulipa malipo yote stahiki kwa wakulima yatakayotolewa na Benki ya

kilimo Tanzania (TADB).

 

“Na

tumeshaandaa fedha zao tunataka wakulima walipwe haraka iwezekanavyo lakini

tumeanza kumjali mkulima kwanza halafu taasisi zingine zinazofaidika na korosho

zitafuata” Alisisitiza

 

Mhe

Hasunga amewapongeza wakulima kwa kuwa wavumilivu katika kipindi hiki cha mpito

wakati serikali ilipokuwa ikitafuta ufumbuzi wa zao la korosho.

 

 

About Alex

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen + 1 =