Tuesday , March 26 2019

Home / SIASA / BREAKING NEWS:MTOLEA APOKELEWA CCM

BREAKING NEWS:MTOLEA APOKELEWA CCM

ALIYEKUWA MBUNGE WA TEMEKE NDG. ABDALAH MTOLEA AOMBA KUJIUNGA NA CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

15 Novemba 2018 Wakati tarehe ya mwisho ya kupokea viongozi wa upinzani wanao omba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikifika leo hii, Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Temeke kwa tiketi ya Chama cha CUF Abdalah Mtolea amejivua uanachama wa CUF na kujiuzuru Ubunge wa Jimbo la Temeke, huku akieleza chanzo kikiwa migogoro isiyoisha katika Chama cha CUF kwa zaidi ya miaka miwili sasa.

Tukio la kujivua uanachama wa CUF na kujiuzuru ubunge lilitokea ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wakati akichangia hoja katika mjadala uliokuwa unaendelea mapema leo. Ndugu Abdalah Mtolea jioni ya leo ametangaza nia yake ya kuomba kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) akieleza msingi wa uamuzi huo ukiwa umejengwa katika ukweli kwamba wengi ya wapiga kura wake wamemshauri kujiunga na CCM.

Akizungumza katika kikao cha waandishi wa habari, watumishi na baadhi ya wanachama wa CCM katika Ofisi ya Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma, Ndugu Mtolea ameeleza sababu zinazopelekea kuomba kujiunga na CCM na kuwa amevutiwa na Mageuzi makubwa ya Kiuongozi na kazi nzuri inayofanywa na CCM na Serikali yake chini ya Ndugu John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kikao hicho cha waandishi wa habari, watumishi na baadhi ya wanachama wa CCM kimehudhuriwa pia na Kamaradi Bashiru Ally, Katibu Mkuu wa CCM ambaye amemwelekeza kwenda katika tawi lililo karibu na makazi yake Wilayani Temeke, Jijini Dar es Salaam ili afuate utaratibu wa kuomba uanachama wa CCM.

Imetolewa na,

IDARA YA ITIKADI NA UENEZI CHAMA CHA MAPINDUZI (CCM)

OFISI YA MAKAO MAKUU DODOMA

About Alex

Check Also

aaa

DKT,BASHIRU KUZINDUA MKAKATI WA KUIMARISHA DEMOKRASIA DODOMA

    Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma, Jamila Yusuph,akitoa taarifa kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nineteen − nine =