Saturday , March 23 2019

Home / BIASHARA / HALOTEL YAZINDUA OFA KABAMBE INAYOKWENDA KWA JINA LA (CHRISTMAS BANG BANG)

HALOTEL YAZINDUA OFA KABAMBE INAYOKWENDA KWA JINA LA (CHRISTMAS BANG BANG)

1

Bw. Mhina Semwenda Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo Victoria jijini Dar es salaam kuhusu ofa ya Krismasi namwaka mpya  waliyoizindua leo inayokwenda kwa jina la Christmas Bang Bang namna itakavyowanufaisha wateja wa aina zote kutoka kampuni hiyo kushoto ni Bi. Hindu Kanyamala Meneja Mawasiliano Halotel.

2

Bw. Mhina Semwenda Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo Victoria jijini Dar es salaam kuhusu ofa ya Krismasi namwaka mpya  waliyoizindua leo inayokwenda kwa jina la Christmas Bang Bang namna itakavyowanufaisha wateja wa aina zote kutoka kampuni hiyo Kulia ni Bi Stella Pius Meneja Uhusiano Halotel.

4

Bw. Mhina Semwenda Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Kampuni ya simu za mkononi ya Halotel akifafanua  jambo wakati akijibu maswali ya  waandishi wa habari katika makao makuu ya kampuni hiyo Victoria jijini Dar es salaam kuhusu ofa ya Krismasi na mwaka mpya  waliyoizindua leo inayokwenda kwa jina la Christmas Bang Bang,  Kushoto ni Bi. Hindu Kanyamala Meneja Mawasiliano Halotel na Kulia ni Bi Stella Pius Meneja Uhusiano Halotel.

…………………………………………………………………………….

Katika kuelekea msimu huu wa sikukuu kampuni ya simu ya Halotel imetoa punguzo la zaidi ya asilimia sitini (60%) katika kifurushi chake cha siku ambapo sasa wateja watapata GB 2 kwa shilingi 2000 ikiwa ni gharama nafuu zaidi ya vifurushi vya intaneti na kutoa punguzo kubwa la smartphone aina ya OXE 101.
Akizungumzia punguzo hilo kubwa, Mkuu wa Mawasiliano wa Halotel, Mhina Semwenda amesema ofa hiyo imezingatia mahitaji makubwa ya wateja wa mtandao huo katika msimu huu wa sikukuu na kutoa nafasi kwa wateja kupeana taarifa na fursa ya kutembelea mitandao mbali mbali ya kijamii.
“Msimu wa sikuu kuu unatoa fursa kwa wateja wetu, kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi, wengi wanahitaji taarifa za maeneo wanayoenda, au wanaweza kupenda kushare matukio au hata kupata muda mwingi wa kutumia simu zao, hivyo tumeonelea ni vyema sasa, tuwape sababu ya kufurahia msimu huu wa sikukuu kwa kuwapatia ongezeko kubwa kabisa la GB za intaneti, Alisema Mhina na kuongeza.
Jambo kubwa kabisa la kuwahakikishia wateja wetu ni kuwa maeneo yote watakayo kwenda iwe vijijini au sehemu nyinginezo, watakuwa pamoja nasi na watakuwa na uhakika wa kutumia huduma zetu kutoka katika mtandao wetu uliosambaa Zaidi hapa nchini kwa kufikia Zaidi ya asilimia 95% ya Watanzania.
“Huduma hii ni zawadi kwa wateja wote wa Halotel nchini msimu huu wa sikukuu kwa kuendelea kutumia intanet yenye kasi zaidi nchini kipindi hiki cha mapumziko wakati wowote, ambapo kwa kujiunga na huduma ya CHRISTMAS BANG BANG mteja atapata  kifurushi cha intenet cha GB 2 cha siku kwa sh 2000 tu tofauti na kirushi cha kawaida ambacho mteja angepata GB 1.3 kwa siku kwa sh 2000.Zaidi tunapenda kuwakumbusha watanzania na wateja wetu wote wataweza kujipatia zawadi mbali mbali  pindi watakapo fika kwenye maduka yetu ya Halotel nchi nzima katika  kipindi msimu huu wa sikukuu. Tunatakia watanzania na wateja wa Halotel waipokee zawadi ya CHRISTMAS BANG BANG kutoka Halotel,. alisema Kanyamala na kuongeza.
Tunawahakikishioa wateja wetu kuwa tutafanya msimu huu wa sikukuu kuwa Bang Bang kwa kuendelea kuboresha huduma zetu.

About bukuku

Check Also

maxresdefault

HOTELI YA KWANZA ARUSHA YATENGA MILIONI KUMI KWA AJILI YA YATIMA

UONGOZI wa hoteli ya kitalii ya New Safari Hoteli ya jijini Arusha umefanikiwa kujiwekea utaratibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × four =