Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / KUANDIKWA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI PWANI KUTEMBELEA MIUNDOMBINU MBALIMBALI

KUANDIKWA AANZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI PWANI KUTEMBELEA MIUNDOMBINU MBALIMBALI

IMG_20181206_122100_6
NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 
UJENZI wa barabara ya km.2 ,kwa kiwango cha lami, utakaogharimu fedha za kimarekani milioni mbili kuelekea, chuo cha uongozi na itikadi cha Mwalimu Julius  Nyerere, Kwamfipa Kibaha mkoani Pwani, unatarajia kuanza mwezi Mei 2019.
Akitembelea ujenzi wa chuo hicho katika ziara yake ya siku mbili aliyoianza mkoani hapo, Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kuandikwa alisema ,wakati ujenzi wa chuo hicho ukiendelea kuna kila sababu ya kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwemo barabara ili kufungua milango ya kimaendeleo na kiuchumi. 
Alieleza, awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara hiyo utajengwa na mkandarasi wa ujenzi wa chuo hicho kampuni ya Crje ya China kama sehemu ya mradi. 
Kuandikwa alieleza, serikali nayo itaendelea kuangalia namna ya kuboresho miundombinu hiyo kwa kufungua barabara zinazoingia kwenda katika chuo hicho. 
“Serikali chini ya Rais Dk. John Magufuli inatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  kwa vitendo, hivyo tutahakikisha wananchi wananufaika na miradi hii mikubwa pamoja na ujenzi wa miradi ya kimkakati “
Aidha Kuandikwa alimtaka mkandarasi, kukamilisha ujenzi wa chuo hicho kwa wakati ili mafunzo yaanze kutolewa kwa muda uliopangwa.
IMG_20181206_123106_3
Nae katibu wa CCM mkoani Pwani Anastazia Amas 
alimuomba kujengwa barabara ya Makofia -Vikumburu kwa kiwango cha lami kutokana na umuhimu wake. 
Mratibu wa mradi ujenzi wa chuo cha uongozi cha mwalimu Julius Nyerere Kwamfipa, Emmanuela Kaganda alisema, ujenzi wa barabara utaanza mwezi mei mwakani baada ya mvua. 
Alisema changamoto iliyopo ni ufinyu wa barabara kutoka njia ya kuingilia kutoka barabara kuu ya Morogoro -Kwamfipa kuelekea chuoni ambapo watashindwa kuondoa makazi ya watu kutokana na kutokuwa na fedha ya kuwalipa fidia. 
Akizungumzia ujenzi wa chuo, Emmanuela alieleza, ulianza July 2018 na mkandarasi anatarajiwa kukamilisha na kukabidhi July -2020

About bukuku

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

four × 5 =