Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / MADIWANI 11 WALIOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU WASUBIRI HATMA YAO

MADIWANI 11 WALIOJIHUSISHA NA UVUVI HARAMU WASUBIRI HATMA YAO

PICHA 1

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina akitoa msimamo wa wizara baada ya kuwasilishiwa taarifa ya ‘Operesheni Sangara II, Mwaka 2018’ kutoka kwa wakuu wa makamanda wa operesheni hiyo (hawapo pichani) Jijini Dodoma.

PICHA 2

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega akitoa maelekezo kwa makamanda wa ‘Operesheni Sangara II, Mwaka 2018’ (hawapo pichani) Jijini Dodoma.

PICHA 3

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama akifafanua jambo kwa makamanda wa ‘Operesheni Sangara II, Mwaka 2018’ (hawapo pichani).

PICHA 4

Baadhi ya makamanda walioshirkiki kikao cha tathmini ya kitaifa ya Operesheni Sangara II, Mwaka 2018 kilichoongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina.

………………………………………………………………………………………..

Na. Edward Kondela, (Wizara ya Mifugo na Uvuvi) Dodoma

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema wizara yake inatafakari hatua za kuchukua kwa madiwani 11, waliokamatwa wakijihusisha na vitendo vya uvuvi haramu, baada ya kukamatwa na makamanda wa ‘Operesheni Sangara II, mwaka 2018’

Mhe. Mpina ameyabainisha hayo Jijini Dodoma (05.12.2018) wakati wa kikao cha tathmini ya kitaifa ya ‘Operesheni Sangara II, Mwaka 2018’ iliyoanza tarehe Tisa Mwezi Oktoba Mwaka 2018, katika Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Bwawa la Mtera na Bwawa la Nyumba ya Mungu, ambapo amelalamikia vitendo vya baadhi ya watendaji wa serikali wakiwemo madiwani, kukwamisha zoezi hilo katika baadhi ya maeneo na kuwataka makamanda wanaofanya operesheni hiyo kutosita kuwakamata viongozi wanaojihusisha na uvuvi haramu. Waziri Mpina amesema

“Tumekamata sasa madiwani na mimi niwapongeze sana mliofanya hilo jukumu, tumekamata madiwani tena wa CCM, na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Chato diwani wa CCM, akishiriki uvuvi haramu, niwape tu taarifa kwamba, wamekuja na hakuna aliyebisha na wote wameendelea kuomba msamaha, ni ushindi mkubwa sana kwa wizara”. Alisema Mhe. Mpina

Katika Hatua nyingine Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mheshimiwa Luhaga Mpina, amesema kutokana na vitendo vya uvuvi haramu kukithiri katika Ziwa Victoria, wizara imedhamiria kuanzisha mahakama inayotembea (Mobile Court) ili kuwachukulia hatua za kisheria watu watakaobainika kuhusika na vitendo hivyo kwa kuwafikisha mahakamani. 

Mpina ameongeza kuwa “Kwa sasa hivi kwa mfano Ziwa Victoria, hatuwezi tena kuzuia ‘Mobile Court’ inabidi tu lazima tuwe nayo, kwa sababu waliobaki wanaendeleza uvuvi haramu kule, ni wale walioshindikana kabisa kwamba sasa hamna njia nyingine zaidi ya kutumia ‘mobile court”. Alisema Mhe. Mpina.

Katika kikao hicho pia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina amesema kutokana na mafanikio makubwa ya operesheni ya kudhibiti uvuvi haramu kwenye Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Bwawa la Mtera na Bwawa la Nyumba ya Mungu, kuna ongezeko kubwa la samaki, hivyo ni wakati wa kuanza kutafuta masoko ya ndani na nje ya nchi. 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewaasa makamanda wanaoshiriki katika uvuvi haramu kutokata tamaa, kutokana na kukosa ushirikiano kutoka kwa baadhi ya viongozi wa serikali na badala yake waendelee kutoa elimu na kutambua baadhi ya maeneo yaliyopitiwa na operesheni hiyo, jambo hilo bado ni jipya.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama aliwaarifu wajumbe wa kikao hicho, wakiwemo makamanda wanaoshiriki katika operesheni ya uvuvi haramu kutobweteka kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika ‘Operesheni Sangara II, Mwaka 2018’ kwa kuwa bado vitendo vya uvuvi haramu vinaendelea kwa kuwa wahusika wanatumia njia mbalimbali za kutekeleza vitendo hivyo. 

‘Operesheni Sangara II, Mwaka 2018’ ilizinduliwa Tarehe Tisa Mwezi Oktoba Mwaka 2018 (09.10.2018), kwa lengo la kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu katika Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Bwawa la Mtera na Bwawa la Nyumba ya Mungu, ambapo watuhumiwa mbalimbali walikutwa na hatia na kupewa adhabu ya kulipa ada mbalimbali, kukamatwa kwa vifaa vinavyotumika katika uvuvi haramu na kutolewa kwa elimu juu ya madhara ya uvuvi haramu kwa wadau wa sekta ya uvuvi.

About bukuku

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

8 + two =