Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / Muhimbili kuendelea kuboresha huduma kwa watu wenye walemavu

Muhimbili kuendelea kuboresha huduma kwa watu wenye walemavu

????????????????????????????????????

Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Comminications Ltd, Maria Sarungi akizungumza kabla ya kufungua huduma ya matibabu bure kwa watu wenye ulemavu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani ambayo ufanyika Desemba 3, kila mwaka. Huduma hiyo inatolewa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na wataalam wabobezi wa hospitali hiyo kuanzia leo hadi kesho.

????????????????????????????????????

Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye maadhimisho hayo leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

????????????????????????????????????

Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dkt. John Rwegasha akizungumza kwenye maadhimisho hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Prof. Lawrence Museru. Kushoto ni Mratibu wa kituo cha Tuje Pamoja kwa Maendeleo ya Jamii, Nadia Baharam, Mkurugenzi wa Kampuni ya Compass Comminications Ltd, Maria Sarungi na Mkurugenzi wa Shirika lisilo la Kiserikali kwa watu wenye ulemavu (PLPDF), Sophia Mbeyela. 

????????????????????????????????????

Mtaalam wa viungo wa Muhimbili, Elieka Kaaya akitoa huduma ya matibabu kwa mtoto mwenye tatizo la ulemavu ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya walemavu duani.

????????????????????????????????????

Mmoja wa watu wenye ulemavu akionyesha bidhaa anazotengeneza.

????????????????????????????????????

Mkurugenzi wa Kampuni ya  Compass Comminications Ltd, Maria Sarungi na baadhi ya wataalam wa afya wa Hospitali ya Taifa Muhimbili.

 ………………………………………………………………………………………………………………..

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) inaendelea kuwatumia watalaam wake wabobezi katika kutoa matibabu yanayolenga kutunza utu, kuepusha magonjwa na ulemavu.

 Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Muhimbili, Dkt. John Rwegasha wakati wa utoaji wa huduma kwa watu wenye ulemavu katika maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu duniani.

 Dkt. John Rwegasha ambaye amemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru amesema katika kufanikisha azma hiyo hospitali imeendelea kukuza huduma zake kwa kuboresha huduma za utengamao (Rehabilitation Services) pamoja na kuendelea kuajiri wataalam mbalimbali wakiwemo watoa tiba kwa vitendo na wafiziotherapia.

 Pia, hospitali imeendelea kuboresha huduma kwa kununua vifaa tiba vya kisasa ambavyo hutumika katika kutoa huduma kwa wagonjwa wenye ulemavu na wasiokua na ulemavu ili wasipatwe na ulemavu wa kudumu.

 “Katika kutimiza wajibu wake kama hospitali na taasisi, Muhimbili tumeendelea pia kutoa ajira kwa watu wenye ulemavu na vilevile tunaboresha majengo yetu ili yawe rafiki kwa matumizi kwa watu wenye ulemavu katika kupata huduma stahiki,’’ amesema Dkt. Rwegasha.

 Akizungumza kabla ya kuzindua utoaji wa huduma, Mkurugenzi wa kampuni ya Compass Communications Ltd, Bi Maria Sarungi amesema watu wenye ulemavu ni sehemu ya jamii hivyo jamii inapaswa kuwajengea uwezo ili waweze kujitegemea na kuendesha shughuli zao za kila siku.

 “Jamii ielewe kwamba watu wenye ulemavu wanaweza kufanya shughuli za maendeleo na kufanikiwa katika maisha na hata kuweza kusaidia watu wengine,” amesema Bi. Maria Sarungi.

 Katika maadhimisho hayo watalaam wametoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa, elimu kuhusu ulemavu wa viuongo pamoja na ulemavu wa akili.

 Akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa Mkuu wa Idara ya Famasia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Deus Buma ametoa rai kwa jamii kuzingatia matumizi sahihi ya dawa ili kuepuka ulemavu ambao unatokea kwa kutumia dawa pasipo kuzingatia ushauri wa watalaam.

 Maadhimisho ya siku ya watu wenye ulemavu Duniani hufanyika kila mwaka Disemba 3, ambapo yalianzishwa na Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1992 kwa lengo la kutetea haki za watu wenye ulemavu ikiwemo kupata huduma bora za fya, kutunza utu na kuchukua maamuzi ya kuwapa uwezo wa kujitegemea katika njanya zote.

 Kauli mbiu ya mwaka huu ni “kuwajengea uwezo, kuwahusisha na kuwapatia haki sawa watu wenye ulemavu.’

 

About bukuku

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen + fifteen =