Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / SERIKALI KUFIKISHA UMEME NANYAMBA MKOANI MTWARA KABLA YA SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2019-DKT KALEMANI

SERIKALI KUFIKISHA UMEME NANYAMBA MKOANI MTWARA KABLA YA SHEREHE ZA MWAKA MPYA 2019-DKT KALEMANI

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa
Mtaa wa Kilimanjaro katika wilaya ya Nanyumbu

Mbunge wa Jimbo la Nanyamba Abasi Chikota akizungumza na wananchi

MKUU wa wilaya ya Nanyamba Evod Mmanda akizungumza

Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani katika akitazama nguzo

Sehemu ya wananchi wakimsikiliza Waziri wa Nishati Dkt Kalemani

Waziri wa Nishati Dkt.Medard Kalemani amesema dhamira yake ni
kuhakikisha huduma ya umeme  inafika katika wilaya ya Nanyamba
mkoani Mtwara kwenye maeneo mengi kabla ya Sherehe za mwaka mpya wa
2019 ili kuweza kutoa fursa ya wananchi kunufaika na huduma hiyo
muhimu kwa maendeleo.

Dkt Kalemani aliyasema hayo
kwenye  mtaa Kilimanjaro wilaya ya Nanyamba mkoani Mtwara wakati
wa ziara yake ambapo alisema  haridhishwi na kasi ya mkandarasi
aliyepewa kazi ya kuunganisha vijiji vya Nanyamba na kusema kuwa
anatoa siku 20 kwa mkandarasi huyo kukamilisha kazi ya kuunganisha
umeme mtaa wa kilimanjaro na maeneo ya jiran hasa kwenye taasisi
zinazohudumia jamii kama hospitali na shule.

“Sijaridhishwa na kasi ya mkandarasi, Sasa leo wakati sisi
tunaondoka mkandarasi yeye atabaki, ili kuhakikisha kabla ya sikukuu
ya chrismas na mwaka mpya umeme Nanyamba unawaka, mkandarasi aweke
magenge yake hapa nataka kazi ifanyike”

Aidha waziri Dkt.Kalemani amelitaka Shirika la Umeme
Tanzania,TANESCO kufungua ofisi katika wilaya ya Nanyamba ili kusogeza
huduma kwa wananchi, ambao wapo tayari kulipia huduma ya Umeme

“Wanamtwara wote ninaimani uwezo wa kulipa ela ya
kuunganishiwa umeme mnayo, hasa kipindi hiki ambacho Serikali inanunua
mazao ya korosho hapa mtwara, hivo naamini wote hapa kwa Sasa uwezo wa
kulipia elfu 27ya umeme mnao”Alisema

Alieleza kutokana na hali hiyo Shirika hilo litafungua ofisi yao
Nanyamba ili kusudi waweze kulipia na kuongeza kuwa vifaa maalum vya
Umeme Tayari (UMETA) 250 vitatolewa kwa wananchi ambao hawana uwezo wa
kutandaza nyaya katika nyumba zao ili waweze kuunganishwa na huduma ya
Umeme.

Waziri wa Nishati Dkt.Medard kalemani yupo
mkoani Mtwara, akifanya ziara ya kikazi ya kukagua maendeleo ya Miradi
ya Umeme vijijini (REA)na kuwataka wananchi kuutumia umeme kama fursa
ya kujiongeZea kipato kupitia biashara mbalimbali

About Alex

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

13 + eight =