Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI UMMY AAGIZA AFISA AFYA WA WILAYA ACHUNGUZWE KWA TUHUMA YA RUSHWA

WAZIRI UMMY AAGIZA AFISA AFYA WA WILAYA ACHUNGUZWE KWA TUHUMA YA RUSHWA

1

Waziri wa Afya, Mhe. Ummy Mwalimu akiteta jambo na Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo wakati wa mkutano wa uhamasishaji kwa kujiunga na mfuko wa Bimba ya Afya

5

 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu akiongea na Wananchi wakati akifanya uhamasishaji kwa Wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya katika mji wa Kitangali Wilaya Newala Mkoa wa Mtwara.

2

Wananchi na Wanachama wa vyama vya Msingi vya Wakulima (AMCOS) waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu alipofika kuhamasisha Wananchi kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika mji wa Kitangali mkoa wa Mtwara.

3

Wananchi na Wanachama wa vyama vya Msingi vya Wakulima (AMCOS) waliojitokeza kumsikiliza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Ummy Mwalimu alipofika kuhamasisha Wananchi kujiunga na mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika mji wa Kitangali mkoa wa Mtwara.

4

Na WAMJW-NEWALA, MTWARA

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Newala Mhe. Aziza Mangosongo, Kumchunguza Afisa Afya wa Wilaya hiyo maarufu kwa jina la Mama Flora kwa tuhuma ya Rushwa aliyochukua kutoka kwa Bw.Shaib Mussa kama adhabu ya kutupa taka hovyo.

Hayo yamefuatia baada ya Mwananchi aliyejitambulisha kwa jina na Shaibu Musa kutoa malalamiko yake mbele ya Mhe.Waziri ya kilipishwa shilingi elfu 50,000 na Bibi Afya huyo mwaka Jana.

Waziri Ummy alisema kuwa Watumishi wa Serikali hasa wa Sekta ya Afya ni lazima wajiepushe na vitendo vya Rushwa na kuacha tamaa zinazopelekea kuminywa kwa haki kwa baadhi Wananchi wanaotaka kupata huduma.

“Namtafuta mmoja ili nimtolee mfano kwa Tanzania nzima, bahati nzuri Mimi ni Mwanasheria, Kosa LA jinai halina muda, hata kama ni 2017, tunataka huyu mtu afuatiliwe, achunguzwe kama kweli shilingi 50,000 iliingizwa kwenye Halmashauri au haijaingia, tunataka Mazingira masafi lakini ile hela iende Serikalini” alisema Waziri Ummy.

Nae Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bw. Bernard Konga amesema kuwa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeanza rasmi kampeni ya uandikishaji ya kijiji kwa kijiji katika Mikoa ya Mtwara na Lindi ili kuwawezesha wananchi hao kuwa kwenye utaratibu mzuri wa kupata huduma za matibabu.

Bw. Bernard Konga aliendelea kusema kuwa, Wananchi wamekuwa wakiingia katika umasikini mkubwa kwa kulazimika kuuza mali za familia kwa lengo la kupata fedha za kugharamia huduma za matibabu.

“Nikuhakikishie Mheshimiwa Waziri na wananchi wote walioko hapa, timu yangu inaanza rasmi kampeni ya kijiji kwa kijini kuanzia wiki ijayo kwa lengo la kumfikia kila mkulima aliyeko katika Mkoa wa Mtwara na Lindi ili wananchi hawa wawe kwenye mfumo bora wa kupata huduma za matibabu wakati wowote, alisema Bw. Konga.

Konga aliendelea kusema kuwa zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wote wako kwenye sekta ya kilimo hususan maeneo ya vijijini na kwa kutambua umuhimu wa kulitunza kiafya kundi hili, Mfuko ulianzisha mpango maalum unaojulikana kwa jina la Ushirika Afya unaowawezesha kujiunga na huduma za NHIF kwa gharama nafuu.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto yupo Mkoani Mtwara kwa ziara ya kukagua hali ya utoaji huduma za Afya Pamoja na uhamasishaji kwa Wananchi kujiunga na mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) na Leo hii yupo Wilayani ya Newala.

About bukuku

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

ten + 15 =