Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / MHANDISI IYOMBE ATUNUKIWA TUZO YA UTUMISHI ULIOTUKUKA

MHANDISI IYOMBE ATUNUKIWA TUZO YA UTUMISHI ULIOTUKUKA

index

Shirika la maendeleo la Japan(JICA) limemtunuku Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandishi Musa Iyombe Tuzo ya Umahiri na Utumishi Uliotukuka.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi Tuzo Mwakilishi Mkuu wa JICA Tanzania Toshio Nagase amesema amekabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya Rais wa Shirika hilo na tuzo hiyo ni ya 14 ambayo hutolewa na Rais wa shirika hilo kwa pamoja na tuzo wanazo toa kwa watu binafsi na mashirika.

Ameongeza kuwa Mhandisi Iyombe anaingia miongoni mwa watu na mashirika 49 waliopatiwa tuzo za shirika hilo lengo ikiwa ni kuwatambua watu binafsi au Taasisi zinatoa mchango wa kipekee na kugusa maisha ya watu katika kuboresha miundombinu, kuendeleza rasilimali watu, kuboresha maisha ya watu pamoja na kupunguza umasikini katika nchi zinazoendelea.

“Mhandishi Iyombe amefanya yote yanayostahili kupata Tuzo hii tangu wakati akiwa anahudumia Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, kisha kuhudumu katika Wizara ya Ujenzi na ndipo kuja hapa OR-TAMISEMI na kote huko alikopita ametoa mchango mkubwa sana katika kuleta maendeleo kwa mtanzania na Taifa kwa ujumla” alisema Nagase.

Aliongeza kuwa mchango wa Iyombe ulianza kuonekana tangu mwaka 1984 mara tu alipomaliza shahada yake ya kwanza ya Uhandishi huko India na kufanya mafunzo kwa vitendo chini ya wataalamu wa Japan waliokua wanajenga barabara ya Kibiti – Lindi.

Kwa kipindi chote cha miaka 34 sasa amejitoa kwa moyo kutumia Taaluma yake ya Uhandishi kushiriki kuhudumu katika miradi mbalimbali ya maendeleo ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania ambayo mingine ilikuwa inasimamiwa na wataalm kutoka Japan.

Akizungumza katika hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka watumishi kufuata nyendo za Mhandisi Iyombe za kuwatumikia wananchi kwa moyo ili waweze kuacha alama ‘Legacy’ katika Utumishi wao wa Umma.

“Tuzo hii anayokabidhiwa Katibu Mkuu wetu leo asingeweza kuipata kama asingekuwa mahiri katika utendaji kazi wake na kujitoa kwa dhati kutatua kero za wananchi; Hii imepelekea yeye kuonekana kati ya wengi kuwa anastahili kutambulika kimataifa, Tuzo hii iwe somo kwetu tuweze kujifunza na kubadilika’ alisema Jafo.

“Nivigumu sana binadamu kumsifia au kuona mazuri ya binadamu mwenzake kama yuko hai lakini leo Mhandisi Iyombe una sifiwa ukiwa hai hii inaonyesha kuwa wewe ni kiongozi wa kuingwa kwani ni vigumu kutambua mazuri ya mtu akiwa hai” Alisema Jafo.

Naye Mhandisi Mussa Iyombe amesema kuwa tuzo hiyo sio yake bali ni tuzo ya watumishi wote kwani ushirikiano wao ndo umemfanya leo anapata tuzo hii kutoka kwa watu wa JICA.

“Siwezi sema tuzo hii ni yangu bali tuzo hii ni yetu sote , nasema hivi kwani hapo nilipo bila ushirikiano wenu mimi ni singeweza kupata tuzo hii, kikubwa namshukuru Mungu na twendelee kumuomba Mungu ili tudumishe ushirikiano wetu katika utekelezaji wa wajibu tulio nao kwa watanzania” Alisema Iyombe.

About Alex

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × five =