Tuesday , March 26 2019

Home / MCHANGANYIKO / KAMISHINA MASAIDIZI WA ARDHI KANDA YA MAGHARIBI AAGIZWA KUONGEZA NGUVU KATIKA CHUO CHA ARDHI TABORA

KAMISHINA MASAIDIZI WA ARDHI KANDA YA MAGHARIBI AAGIZWA KUONGEZA NGUVU KATIKA CHUO CHA ARDHI TABORA

1

Brass Band ya Chuo cha Ualimu Tabora ikiongoza maandamano ya Wahitimu wa Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) kuingia katika viwanjani kwa ajili ya Mahafali ya 36 ya Chuo hicho yalifanyika jana mjini Tabora.

2

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mathias Kabundunguru (aliyeweka mkono kifuani) akishiriki kuimba wimbo wa Taifa wakati wa sherehe za mahafali ya 36 ya Chuo cha Ardhi Tabora zilizofanyika jana.

3

.Mkuu wa Chuo cha Ardhi Tabora (ARITA) Biseko Musiba(aliyesimama) akitambulisha wageni mbalimbali wakati wa mahafali ya 36 ya Chuo hicho yaliyofanyika jana mjini Tabora.

4

Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Ardhi Tabora(ARITA) wakimsikiliza Mgeni rasmi wakati wa mahafali ya 36 ya Chuo hicho yalifanyika jana.

5

Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ardhi Tabora(ARITA) Profesa Gabriel Kassenga akitoa salamu za Bodi wakati mahafali ya 36 ya  ARITA yaliyofanyika jana.

6a

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mathias Kabundunguru akiwahutubia wahitimu wa mahafali ya 36 ya Chuo cha Ardhi Tabora jana.

7

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mathias Kabundunguru (mwenye Joho la bluu waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali na wakufunzi wa Chuo cha Ardhi Tabora jana mara baada ya kumalizika kwa mahafali ya 36 Chuo cha Ardhi Tabora yaliyofanyika jana.

………………………………………………………………………

NA TIGANYA VINCENT- TABORA

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi  Mathias Kabundunguru amemwagiza Kamishina Msaidizi wa Ardhi Kanda ya Magharibi kutumia muda wake wa ziada kuomba vipindi vya kufundisha katika Chuo cha Ardhi Tabora ili kusaidia kukabiliana na tatizo la upungufu wa wakufunzi Chuoni hapo.

Alisema kuwa ni vema Kamishina huyo akatumia muda ambao anakuwa hana majukumu ya kiofisi kama vile siku ya Jumamosi kutoa mchango wake kwenda kusaidia wakufunzi katika kufundisha.

Kabundunguru alitoa kauli hiyo jana wakati wa sherehe za mahafali ya 36 ya Chuo cha Ardhi Tabora(ARITA).

Alisema hatua hiyo pia itasaidia kujikumbusha mafunzo aliyopata wakati akiwa Chuoni na kuhamisha ujuzi huo kwa wanachuo wa Tabora.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi, Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Ardhi Tabora Profesa Gabriel Kassenga alisema kuwa ARITA inakabiliwa ufinyu wa bajeti ambayo inayosababisha Mpango Kabambe wa Chuo wa miaka kumi kutekeleza kwa asilimia 30 .

Alisema hali hiyo imesababisha Chuo hicho kukabiliwa na  uhaba wa watumishi hasa wakufunzi katika kozi mbalimbali zinazofundishwa Chuoni hapo.

Profesa Kasenga alisema kuwa hatua hiyo imewafanya kuwa na  na mzigo mkubwa katika kutekeleza majukumu yao ya  ufundishaji.

Mwenyekiti huyo aliomba Serikali kuongeza tengeo la bajeti kwa ajili ya kukamilisha Mpango Kabambe wa Chuo wa miaka 10 ili asilimia 70 zilizobaki ziweze kukamilika.

About bukuku

Check Also

AA

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 − seven =