Tuesday , March 26 2019

Home / SIASA / MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI

MNEC RATCO AKEMEA MAKUNDI,MIGOGORO KWA WANA CCM WILAYANI HANDENI

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco
akizungumza na wajumbe cha Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi
wilaya ya Handeni wakati wa ziara yake ya kujitambulisha ambapo
alisisitiza umoja na mshikamano itakayofanyika mkoa mzima wa
Tanga

Mjumbe wa Halmashauri ya Halmashauri Kuu ya
CCM Taifa Mwalimu Mwantumu Zodo akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia
ni
MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga (MNEC)
Mohamed Salim alimaarufu Ratco kushoto ni Katibu wa UVCCM Mkoa wa
Tanga Zawadi Nyambo
   
         

MKUU wa wilaya ya Handeni Mkoani Tanga Godwin Gondwe akizungumza
wakati wa ziara hiyo.

 MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani
Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco wa pili kutoka kulia akiwa
na 
Mjumbe waHalmashauri ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mwalimu Mwantumu Zodo
wakisikiliza hoja mbalimbali za wanachama

 Sehemu ya wanachama wa CCM wilayani Handeni wakimsikiliza MNEC

  MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani
Tanga (MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco katikati akiwa kwenye
picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kikao hicho kushoto ni
Mjumbe wa Halmashauri ya
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Mwalimu Mwantumu Zodo kulia ni Katibu wa
CCM wilaya ya Handeni
Salehe Kikweo


MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa Mkoani Tanga
(MNEC) Mohamed Salim alimaarufu Ratco amewataka wanachama wa chama
hicho wajiepushe na migogoro, makundi na majungu yasiyokuwa na tija
kwa ustawi wa chama chao kwani yanaweza kusababisha mpasuko miongoni
mwao.

Salim alitoa wito huo wakati wa ziara yake ya kujitambulisha na
kuzungumza na wajumbe katika kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi wilaya ya Handeni ambapo alisema kwa sasa wanachama hao
wanatakiwa kubadilika na kutokuipa nafasi kwani inaweza kurudisha
nyuma maendeleo.

Alisema suala hilo limekuwa likimuumiza sana huku akiwataka wanachama
kuhakikisha wanaachana nayo ili waweze kuunganisha nguvu za pamoja
katika kukijenga chama chao ili kiendelee kuwa imara na kuendelea
kuwatumikia watanzania.

“Ndugu zangu labda niwaambie kwamba mimi naumizwa sana na migogoro
ambayo imekuwa ikijitokeza kwani haina tija kwa ustawi wa chama chetu
na inaweza kutugawa sisi hivyo niwatake msiipe nafasi kwenye maeneo
yenu tuungane kwa pamoja tushirikiana kwa lengo la kuhakikisha haipewi
nafasi “Alisema Mnec huyo.

Aidha pia aliwataka wajumbe hao kuwatumikia wananchi bila kubaguana
rangi, jinsia ikiwemo kushuka chini kufanya kazi na wenzao waliowapa
dhamana hiyo muhimu ili kuweza kusogeza mbele gurudumu la maendeleo
kwao na jamii zinazowazunguka.

“Katika uchapaji kazi wetu tuige mfano wa Rais wetu mpendwa Dkt John
Magufuli ambaye amekuwa akifanya mambo makubwa na yenye maendeleo kwa
watanzania na hivyo kupelekea kuinua uchumi wa nchi  …lakini
niwaambie kwamba uwepo wa CCM kushika dola  hata wafanyabiashara
na watu wengine wanaofanya shghuli zao kwa amani na utulivu,

“Niwaambie kwamba katika awamu zote tano ni nzuri lakini hii tulionayo
ilipelekea mimi kuvutiwa na kugombea nafasi hiyo ya Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya CCM Taifa nilikuwa kwenye chama muda mrefu kutoka
mfumo wa vyama vingi ulipoanza lakini baada ya kuona Mwenyekiti wao wa
Taifa analipigania sana Taifa na kutoa maamuzi yenye tija kwa ustawi
wa maendeleo ya nchi yetu ndipo nilipoona tunapaswa kumuun ga mkono
“Alisema.

Pia aliwaaambia wajumbe hao kwamba wanapotafuta nafasi kwa njia ya
demokrasia na inapotokea bahati mbaya mwenzako kura zake hazikutosha
naombeni muweka moyo wenu safi kwa kushirikina na wenzanu waliopata
ridhaa.

Katika hatua nyengine Mjumbe huyo wa Halmashauri Kuu ya Chama cha
Mapinduzi Taifa Ratco alimuagiza katibu wa CCM wilaya ya Handeni
kuhakikisha miradi ya chama hicho wanaiorodhesha ili aweza kutambua
ipo mingani na nini kinapatikana ili waweze kusaidiana katika
kusimamia mradi iweza kutatua kero zao zinazowakabili.

Naye kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya
Handeni Salehe Kikweo alisema kwamba chama wilayani humo kinawanachama
60015 ambapo kati ya wao wanaume ni 29990 na wanawake ni 30025 huku
akieleza wanaendele kuhakikisha ilani CCM inatekelezwa na wilaya hiyo
kufanya vizuri kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2019
na  uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020

Alisema mkakati wa CCM wilaya ni kuhakikisha wanazidi kufanya vizuri
kutokana na kwamba wilaya hiyo ni ngome ya CCM ikiwemo kuaanda semina
kwa viongozo huku mambo ya kiuchumi yakiibuliwa ili kukiimariusha
chama kuelekea kwenye uchaguzi

About bukuku

Check Also

aaa

DKT,BASHIRU KUZINDUA MKAKATI WA KUIMARISHA DEMOKRASIA DODOMA

    Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Dodoma, Jamila Yusuph,akitoa taarifa kwa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen + nineteen =