Tuesday , March 26 2019

Home / MCHANGANYIKO / TANESCO yapewaTuzo Ukaguzi wa Mahesabu Nchini kwa Mwaka 2018

TANESCO yapewaTuzo Ukaguzi wa Mahesabu Nchini kwa Mwaka 2018

NAMBA MBILI

Kutoka Kulia  Afisa  Mkuu wa Fedha wa Shirika la Umeme Nchini Tanesco Bi RENATHA NDEGE akionesha Tuzo ya Ushindi iliyotolewa na  Bodi  ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu za Mapato ( NBAA) Kwa TANESCO Baada ya Kuibuka  Mshindi Kwenye Utunzaji na Utengenezaji wa  Hesabu za Fedha  Kwa  Kufuata taratibu  zote.

NAMBA MOJA

Baadhi  Wafanyakazi  wa Shirika la Umeme TANESCO wakifurahia Ushindi wa Tuzo iliyotolewa na Bodi  ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu za Mapato ( NBAA) Kwa TANESCO Baada ya Taasisi  hiyo ya Serikali Kuibuka  Mshindi wa Kwanza  Kwenye Utunzaji na Utengenezaji wa  Hesabu za Fedha  Kwa  Kufuata taratibu  zote.

NAMBA TATU

Tuzo ya Ushindi  wa Kwanza ambayo Shirika la  Umeme TANESCO imepokea  Kutoka  Kwa  Bodi  ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu za Mapato ( NBAA) Kwa TANESCO Baada ya Kuibuka  Mshindi Kwenye Utunzaji na Utengenezaji wa  Hesabu za Fedha  Kwa  Kufuata taratibu zote za Masuala ya  Uhasibu.

……………………………………………………………………….

Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu za Mapato (NBAA) imetoa Tuzo kwa Taasisi za Serikali, makampuni pamoja na mashirika yaliyofanya vizuri kwa mwaka 2018 zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya utoaji wa tuzo hizo, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Ashatu Kijaji ameeleza kuwa lengo la NBAA  ni kuendelea kuwapa moyo wakaguzi na wahasibu mbalimbali kwa kukuza hali ya kujituma na kuwajibika kwa makampuni na mashirika hayo ikiwa ni chachu ya kuongeza ufanisi na ushindani kwa Taasisi hizo.

Aidha, Mhe. Kijaji ameipongeza Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu kuendelea kuandaa Tuzo hizo na kuona haja ya kuongeza vipengele kwa washiriki, na kusema lengo la NBAA ni kukuza hali ya kujituma kwa Taasisi mashirika pamoja na kuandaa taarifa ya fedha  zilizo na viwango vya kimataifa.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Uhasibu na Ukaguzi wa Hesabu za Mapato (NBAA) Bw. Pius Maneno amesema kuwa washindi wa Tuzo hizo wamepatikana kupitia mchakato uliofanywa na wakufunzi wa taaluma ya Uhasibu Nchini ambao wanaangalia vigezo vikiwemo kuwa na hati safi na kuwasilisha hesabu kwa wakati na pia kufikia viwango vya ubora wa taarifa pamoja na asilimia 75 ya mapato kwa mwaka 2018.

Kwa upande wao Shirika la Umeme nchini (TANESCO) ambao ni Washindi wa tuzo ya kutunza mahesabu na kutengeneza mahesabu kwa kufata taratibu zote wameishukuru sana NBAA kwa kushinda tuzo hiyo kwani ni mwaka wa pili sasa wamekuwa wakishinda tuzo hiyo.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo,Afisa Mkuu wa Fedha kutoka Shirika la Umeme (TANESCO) Bi. Renatha Ndege ameeleza kuwa ushindi wa tuzo hiyo unadhihirisha kuwa Shirika lao linaaminika sana kwa watanzania kwa kuzalisha umeme wa uhakika na kuweza kushika nafasi ya pili kwa mashirika ya umma na kuahidi kuendelea kuandaa mahesabu yaliyobora na makini kwa miaka ijayo mengine.

Nae Naibu Mkurugenzi Mtendaji upande wa uzalishaji, Mhandisi Abdalah Ikwasa ameeleza kuwa Shirika Hilo la umeme bado linafanya kazi kwa ufanisi mzuri zaidi na hivyo kuwafanya kuweza kushinda kwa mara nyingine zaidi.

About bukuku

Check Also

AA

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

16 − 4 =