Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / Mashine Mpya ya Utrasound kuwanufaisha Watoto Wachanga Muhimbili

Mashine Mpya ya Utrasound kuwanufaisha Watoto Wachanga Muhimbili

 

uchangiaji 1

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akipokea mashine ya Ultrasound kutoka kwa  Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto Antke Zuechner wa  Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya  Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiograph). Thamani ya mashine hiyo ambayo itatumika kwa watoto ni shilingi milioni 34

Uchangiaji 2

Mhandisi wa vifaa tiba Evance Swai kutoka Pacific diagnostic akiwaonyesha madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja na Naiz Majani jinsi mashine ya Ultrasound ambayo imetolewa na  Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya  Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) inavyofanya kazi. Mashine hiyo itatumika kwa ajili ya  kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiograph) kwa  watoto wenye matatizo ya moyo ni thamani yake ni shilingi milioni 34.

uchangiaji 3

Madaktari bingwa wa magonjwa ya moyo kwa watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Sulende Kubhoja na Naiz Majani wakiangalia  mashine ya Ultrasound ambayo imetolewa na  Jamii ya Ujerumani kwa magonjwa ya watoto ya  Ukanda (Germany Society for tropical pediatrics) ambayo itatumika kwa ajili ya  kipimo cha kuangalia jinsi moyo unavyofanya kazi (Echo Cardiograph) kwa watoto wenye matatizo ya moyo.

Picha na JKCI

………………….

 

Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) leo imepatiwa msaada wa mashine ya kisasa ya Utrasound ambayo itatumika katika wodi ya watoto wachanga kwa ajili ya kuwafanyia vipimo vya moyo, kichwa na tumbo.

Mashine hiyo yenye teknolojia ya juu na uwezo mkubwa wa kuchunguza magonjwa hayo ina thamani ya dola za kimarekani 17,000 imetolewa na Taasisi ya Kijerumaini inayoitwa The German Society for Tropical Paediatrics (GTP).

Akipokea msaada huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Lawrence Museru, Mkuu wa Kitendo cha Sheria katika hospitali hiyo Bi. Veronica Hellar amesema mashine hiyo imetolewa maalum kwa ajili ya kuwahudumia watoto wachanga hivyo itatumika kama ilivyokusudiwa.

“Tunashukuru kwa msaada huu mliotupatia ambao umekuja wakati muafaka hasa ukizingatia lengo la hospitali ni kuendelea kuboresha huduma ya afya ya mama na mtoto,” amesema Bi. Hellar.

Kwa upande wake muwakilishi kutoka taasisi hiyo Dkt. Antke Zuechner amesema msaada huo una lenga kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Muhimbili katika kuhudumia watoto wachanga.

Watalaam wa MNH watapatiwa mafunzo maalum ili kuweza kutumia mashine hiyo ambayo ni ya kisasa zaidi.

About Alex

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

18 − seven =