Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / SERIKALI KUBORESHA NA KUPANUA HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJITAKA KATIKA JIJI LA MWANZA

SERIKALI KUBORESHA NA KUPANUA HUDUMA YA MAJISAFI NA MAJITAKA KATIKA JIJI LA MWANZA

1

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akiwa na Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Ilemela, Anna Mbawala katika tenki la maji la Mradi wa Maji Igongwe, mkoani Mwanza

2

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso akitoka kukagua ujenzi wa tenki la maji la Mradi wa Maji wa Nyasaka, wilayani Ilemela katika Mkoa wa Mwanza

3

Naibu Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (kushoto) akiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka jijini Mwanza (MWAUWASA), Mhandisi Anthony Sanga (katikati) na Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Agelina Mabula katika ziara ya kukagua miradi ya maji katika Wilaya ya Ilemela, mkoani Mwanza

4

Mafundi wakiendelea na kazi ya ujenzi wa chanzo cha Mradi wa Maji wa Igombe katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, mkoani Mwanza.

…………………………………

Serikali imeanza kuchukua hatua  ya kuboresha na kupanua huduma ya majisafi na majitaka katika jiji la Mwanza kwa  wananchi wanaoishi milimani na pembezoni mwa jiji hilo kwa nia ya kumaliza kero katika  maeneo hayo ambayo kwa muda mrefu yamekuwa na changamoto ya huduma hiyo.

Hayo yamebainika katika ziara ya  Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso  (Mb) katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela  na kuridhishwa na kazi inayofanywa na mkandarasi kampuni ya Jos Hansen & Soehne GmbH/JR International  Bau GmbH kutoka Ujerumani kupitia usimamizi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Mwanza (MWAUWASA). Gharama ya mradi huo ni kiasi cha Shilingi  bilioni 38.927.

Waziri Aweso amesema mradi huo utaboresha na kupanua  huduma ya majisafi katika maeneo ya milimani hususani maeneo yaliyo juu ya matenki  ya maji ambayo hayapati huduma kwasasa ambayo ni Nyasaka, Bugarika, Nyegezi, Capripointi, Mjimwema, Nyakabungi na Kitangiri.

Ameongeza kuwa mradi huo utahusisha uboreshaji na upanuzi wa mfumo wa majitaka kupitia usambazaji wa mabomba mapya  na kubadilisha ya zamani yaliyochakaa katika maeneo ya Mabatini A na B, Kilimahewa, Isamilo, Igogo, Barabara ya Kenyata na Makongoro. Pamoja na kuongeza ufanisi wa mitambo ya kusukuma majitaka katika kituo cha  Makongoro, Kirumba na Mwanza South.

Vilevule ameitaka MWAUWASA kusimamia  mradi huo vizuri na ukamilike kwa wakati na wizara itahakikisha fedha zinapatikana  kwa wakati.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa MWAUWASA  Mhandisi Antony Sanga amesema mradi huo unatarajia kukamilika mwezi Aprili 2019 na mpaka hadi Disemba 15 2018 utekelezaji wake ulikua umefika asilimia 60. Mradi huo utakapokamilika utanufaisha  zaidi ya wakazi laki moja waishio katika maeneo ya jiji la Mwanza kwa tathmini ya hadi kufikia mwaka 2028.

About Alex

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × 5 =