Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / UPUNGUFU WA MADARASA WASABABISHA WANAFUNZI 2610 KUTOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA DODOMA

UPUNGUFU WA MADARASA WASABABISHA WANAFUNZI 2610 KUTOJIUNGA KIDATO CHA KWANZA DODOMA

RC DODOMA JUNI

Na.Alex Sonna,Dodoma

Wanafunzi 2610 kati ya 8038 waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwa mwaka 2019 katika Halmashauri ya jiji la Dodoma wameshindwa kujiunga na masomo kutokana tatizo la  upungufu wa vyumba vya madarasa.

Haya yamesemwa  leo Januari 10, 2019 kabla ya kuanza ziara ya kutembelea shule zenye upungufu huo Mkuu wa mkoa wa Dodoma Dk Binilith Mahenge hatokubali kuona halmashauri yoyote ndani ya Mkoa ikihangaika na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika hatua za mwishoni baada ya wafanzi kufaulu.

“Yapo mambo ambayo tusikubali kuyafanya dakika za mwisho kwa mfano vyumba vya madarasa , matundu ya vyoo na madawati, sababu tunajua wale watoto wanaofanya mtihani mwezi wa tisa wapo watakaofaulu na watachaguliwa na watahitaji vyumba vya madarasa , vyoo vyumba za waalimu na vitu vingine,” alisema na kuongeza.

“Sasa maelekezo yangu ni kuwa vyumba vyote vinatakiwa kukamilika ikiwa ni pamoja na hivyo 10 viingine kwenye mpango maana, ukiacha vyumba 10 umewaacha wanafunzi 500, na kuanzia sasa sitakubali katika mkoa wangu kuona halmashauri inahangaika dakika za mwisho,” amesema Dk Mahenge.

Hata hivyo alimuagiza Mkuu wa wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi kuhakikisha anakaa na viongozi wa serikali za mitaa ili wakawahamasishe wananchi kutambua umuhimu wa watoto wao kuripoti katika shule walizochaguliwa.

“Na kwa sababu kila kata kuna shule hivyo mtakuwa mmepata orodha ya wanafunzi walichaguliwa na wajaripoti hivyo muwaelekeze wenyeviti wa serikali za mitaa kwamba watoto hao waripoti shuleni na kwamba wasiporipoti nafasi zao zitachukuliwa na wanafunzi wengine ambao waliafauli lakini wamekosa nafasi yakuchaguliwa kutokana na upungufu wa madarasa,” alisema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya jiji la Dodoma hapa Hidaya Maeda alisema wamamua kijenga madarasa 40 badala ya 52 yanayohitajika kulingana na fedha zilizotolewa.

“Ni kweli mahitaji yetu ni madarasa 52 lakini kwa mpango wa haraka wa sasa ni kwamba tumejipangia kukamilisha madarasa 40, kwa maana tunapewa mgao kila kota kwa hiyo kota hii ya januari kuna hela nyingine tutapewa hivyo tutakamilisha hayo madarasa mengine,kufikia februari 9, 2019 yawe yamekamilika

About Alex

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × 5 =