Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI UMMY ACHANGIA TOFALI 3500,SARUJI MIFUKO 250 UJENZI WA MADARASA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA

WAZIRI UMMY ACHANGIA TOFALI 3500,SARUJI MIFUKO 250 UJENZI WA MADARASA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI TANO JIJINI TANGA

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akilakiwa na wanafunzi wa shule ya Sekondari Pongwe Jijini Tanga wakati alipokwenda kuwakabidhi matofali na mifuko ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kushoto akikagua madarasa kwenye ambayo hayajakwisha kwenye shule ya Sekondari Pongwe kabla ya kuwakabidhi mifuko ya saruji na matofali  kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa na kushoto ni Diwani wa Kata ya Pongwe(CCM) Mbaraka Sadi
Diwani wa Kata ya Pongwe(CCM) Mbaraka Sadi akizungumza kulia ni MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu
MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi mifuko ya saruji Diwani wa Kata ya Pongwe (CCM) Mbaraka Sadi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasaa kwenye kata yake
sehemu ya mifuko ya saruji ilioyotolewa na Waziri Ummy

Sehemu ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Pongwe wakifuatilia hotuba ya MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu katika akiwa kwenye picha ya pamoja na walimu wa shule ya Sekondari Pongwe

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akiwa katikati ya wanafunzi wa shule ya Sekondari Mikanjuni mara baada ya kukabidhi msaada wa matofali na mifuko ya saruji

Sehemu ya wananchi wakifuatilia matukio kwenye hafla hiyo

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoani Tanga(CCM) na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu kulia akimkabidhi Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Daudi Mayeji sehemu ya matofali aliyotoa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ili wanafunzi wapata fursa ya kusoma

Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Tanga na Waziri wa
Afya, Ummy Mwalimu leo amekabidhi matofali 3,500 zenye thamani ya shilingi
milioni 5.6 na mifuko ya Saruji 250 yenye thamani ya shilingi milioni 3 ili kuweza kusaidia kutatua tatizo la uhaba wa madarasa.

Msaada huo aliuta  kwa ajili ya ujenzi wa Madarasa ya Sekondari zilizopo katika Jiji la
Tanga ambazo ni Shule za Sekondari   Pongwe, Maweni,
Mikanjuni, Horten na Kiomoni ambapo kila shule imepatiwa Matofali 700 na
saruji mifuko 50.


Akizungumza ktk makabidhiano hayo yaliyofanyika katika Shule
ya Sekondari Mikanjuni, Waziri Ummy ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Tanga (CCM)alieleza kufurahishwa na jitihada za
Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli za kuboresha Elimu nchini na katika Jiji la Tanga
Alisema juhudi hizo zimesaidia  kuwezesha uwepo wa idadi kubwa ya wanafunzi
waliofaulu kujiunga na Elimu  ya Sekondari katika Jiji la Tanga.
 Hivyo
yeye kama mbunge ameona anao wajibu wa kuchangia ujenzi wa madarasa ili
kuwezesha watoto wote 6,024 wa Jijini Tanga waliofaulu Elimu ya Msingi
kuendelea na Elimu ya Sekondari.


Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Tanga  Tobias
Mwilapwa alisema katika mwaka huu 2019 jumla ya wanafunzi 6,024
wamefaulu kuendelea na masomo ya kidato cha kwanza katika Jiji la Tanga
kutoka wanafunzi 5,332 mwaka 2018. 
Hali hii imesababisha mahitaji zaidi
ya Vyumba vya madarasa 71 ili kumudu kuchukua ongezeko la wanafunzi
1,324 waliofaulu kwenda Sekondari katika Jiji la Tanga.


Makabidhiano hayo yamehudhuriwa na Katibu wa CCM Wilaya ya
Tanga Ndugu Kidima, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga, Bwana
Daudi Mayeji, Waheshimiwa Madiwani wa Kata husika, Watendaji wa Idara ya
Elimu na Bodi za Shule husika.


About Alex

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

18 + 3 =