Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / KITILYA ASOMEWA TENA MASHTAKA MAPYA 58

KITILYA ASOMEWA TENA MASHTAKA MAPYA 58

kitilya-1024x576
MAHAKAMA  ya Hakimu Mkazi Kisutu imemsomea mashtaka mapya 58 yakiwemo ya utakatishaji  fedha na kuisababishia serikali hasara ya dola milioni sita aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA, Harry Kitilya na wenzake wawili ambao ni, aliyekuwa Miss Tanzania 1999 Shose Sinare na Sioi Solomon baada ya mapema leo asubuhi kuwafutiwa mashtaka nane yaliyokuwa yanawakabili.
Hata hivyo katika mashtaka mapya TAKUKURU imewaongeza watuhumiwa wawili kwenye kesi hiyo ambao ni  Bedason Shallanda  ambaye ni Kamishina wa  uchambuzi wa  madeni kutoka Wizara ya Fedha  na msaidizi wake Alfredy  Misana.
Katika kesi hiyo mpya washtakiwa wanakabiliwa na  na mashtaka matatu ya kughushi, mashtaka mawili ya kutoa nyaraka za uongo, shatka moja la kujipatia pesa takribani dola milioni mia sita kwa njia za udanganyifu shtaka moja la kutoa nyaraka za uongo kwa lengo la kumdanganya Katibu Mkuu Wizara ya fedha, shtaka moja la kuongoza uhalifu, mashtaka 49 ya  utakatishaji fedha na shtaka moja la kuisababishia Serikali hasara ya dola milioni  sita.
Akisoma mashtaka hayo wakili wa wa Serikali Mkuu Hasan Ngole amedai mbele ya hakimu mkazi mfawidhi Agustina Mmbando kuwa kati ya Machi 15,2013 na Januari 10 2014 ndani ya jiji la Dar es salaam kwa nia ya kudanganya washtakiwa wote walijipatia USD milioni sita kutoka Serikali ya Tanzania wakionyesha kuwa fedha hizo zilikuwa ni malipo ya ada ya uwezeshaji wa upatikanaji wa mkopo na zililipwa  kupitia kampuni ya  EGMA Ltd na benki ya Stanbic 
Aidha, miongoni mwa kosa la utakatishaji fedha inadaiwa washtakiwa wote walilitenda March 18, 2013 na January 10, 2014 wakiwa jijini Dar es Salaam ambapo walitakatisha USD 6,000,000 kwa kuzitoa fedha hizo kupitia njia ya benki kwa jina la Enterprises Growth Market Advisors (EGMA) katika benki ya Stanbic Tanzania.
Pia katika kosa la kusababisha hasara kwa serikali, wanadaiwa kwa pamoja walilitenda kosa hilo Mei 1, 2012 na Juni 1, 2015 wakiwa jijini Dar es Salaam walijipatia USD Milioni 600, 000,000 kama ada ya mkopo uliochukuliwa na Serikali ya Tanzania kutoka katika asilimia 1.4 hadi 2.4 na kusababisha serikali ipate hasara ya USD Milioni 6,000,000.
Baada ya kusomewa mashtaka hayo washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu chochote kwa sababu mahakama haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, wakili Ngole amesema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kesi hiyo imeahirishwa hadi January 24, 2019

About Alex

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 + three =