Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / *MIAKA 3, NDEGE 6, TANZANIA MPYA*

*MIAKA 3, NDEGE 6, TANZANIA MPYA*

5

Na Emmanuel J. Shilatu

Napenda kuungana na Mamilioni ya Watanzania kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli Kwa hatua nyingine ya kununua ndege Mpya ya Airbus A220 – 300 iliyopewa jina la Ngorongoro.

Ndege Ngorongoro Ni Airbus ya pili kutua nchini. Ya Kwanza ni Airbus Dodoma. Tukumbuke ndege Aina ya Airbus Ni ndege ya Kwanza kabisa Afrika inayomilikiwa na Watanzania. Hiyo ni alama isiyofutika iliyoandikwa na Rais Magufuli kwa Tanzania, Afrika na Dunia Kwa ujumla.

Tukumbuke ndege iliyotua Leo Ni ya sita kununuliwa na Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli. Ndege nyinginezo no Bombardier Q400 ambazo zipo 3, Dreamliner 1, na Airbus A220 – 300 ambazo zipo 2. Jumla kuu Ni ndege 6, bado ndege moja.

Ndege hizo zitasaidia kukuza utalii, kuitangaza nchi yetu Tanzania, kukuza biashara, kuongeza mapato ya ndani ambayo yataimarisha uwezo wa ndani wa Serikali kuwahudumia Wananchi na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Tunachojivunia Kwa Rais Magufuli sio tu ndege 6 bali ameweza kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi mpaka sekondari; kujenga miundombinu Kama flyovers; ujenzi wa reli ya kisasa kwa kiwango Cha standard gauge inayotumia umeme; ujenzi wa viwanda vipya zaidi ya 3000; ujenzi wa vituo vya afya vipya pamoja na madarasa.

Mengineyo Ni ongezeko la mapato ya ndani kutoka Tsh. Billion 800 Hadi Trillion 1.3; Ongezeko la wastani wa asilimia 1.5 ya ukuaji wa uchumi nchini; Ongezeko la Tsh. Billion 107 ya makusanyo ya mapya ya madini nchini; Ujenzi was strigler’s gogle itakayozalishi zaidi ya megawats 2100.

Hayo ni kwa uchache zaidi ya Mambo mema yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Magufuli. Hakika huyu ndio Rais Watanzania tuliokuwa tukimwitaji zaidi.

*Shilatu E.J*

About Alex

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × five =