Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / NAIBU WAZIRI AWESO AZINDUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA BULEMBO MISENYI ULIOJENGWA NA WORLD VISION

NAIBU WAZIRI AWESO AZINDUA MRADI WA MAJI KIJIJI CHA BULEMBO MISENYI ULIOJENGWA NA WORLD VISION

Shirika lilislokuwa la Kiserikali la World Vision limendeleza utaratibu wake wa Kusaidia Jamii Katika mambo mbali mbali, Ambapo Shirika Hilo Mkoani Kagera limeongeza mradi mwingine wa maji katika kata ya Bulembo Kijiji Bulembo Halmashauri ya Wilaya Missenyi.

Mradi huo uliogharimu Zaidi ya Shilingi Milioni 150 umejengwa na Mradi wa Missenyi AP kwa kushirikiana na Jamii ya Kijiji Bulenmbo, umezinduliwa na kukabidhiwa kwa Wananchi hao na Naibu Waziri wa Maji MH. Jumaa Aweso (MB) akiwa katika Ziara yake ya Kikazi Wilayani Missenyi Mkoani Kagera.

Mh. Aweso katika  salamu zake akiongea na wananchi amewataka kukilinda chanzo hicho na Mradi huo wa maji Huku akiwataka watumishi Ndani ya Wizara hiyo kuiga mfano na kujifunza namna ya usimamizi wa shughuli hizo kwa kubana Fedha, lakini kazi yenye matokeo chanya.

b1

Mradi wa Maji uliozinduliwa na Mh. Aweso Naibu waziri wa Maji, ukiwa umegharimu zaidi ya Milioni 150 ukiwa umejengwa na World Vision Missenyi AP.

b2

 Ben. Victor kutoka World Vision akifafanua jambo kwa Naibu Waziri Aweso Jumaa hayupo pichani kuhusu mradi huo.

b01

MH. Aweso Naibu Waziri wa Maji akifungua koki ya Bomba LA Maji kuashiria Uzinduzi wa mradi huo

b001

Mh. Aweso Jumaa akitekeleza vyema Kampeini ya Kumtua mama Ndoo kwa Vitendo mara baada ya kuuzindua mradi huo kata ya Bulembo Kijiji Bulembo Halmashauri ya Wilaya Missenyi.

index

Mh Aweso  Jumaa akiwa amejitwisha Ndoo na akicheza ngoma na wananchi kuashiria Uzinduzi wa Mradi wa Maji Bulembo Missenyi

index

Picha ya Pamoja ya Viongozi wa Kijiji, wawakilishi wa shirika la World Vision wakiwa na Naibu Waziri wa Maji Mh. Jumaa Aweso.

About bukuku

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

12 − 6 =