Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege.

NIT Yazindua Kozi ya Wahudumu Ndani ya Ndege.

n1

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe wakatikati aliyekaa akiwa katika picha ya pamoja na viongozi pamoja na waalikwa wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu wa ndani ya ndege iliyozinduliwa jana.Katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT).

n2

Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zakaria Mganilwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya kozi ya uhudumu wa ndani ya ndege, wakati wa uzinduzi wa kozi hiyo leo jijini Dar es Salaam.

n3

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe wakatikati aliyekaa w
kwenye viti akiwa katika picha ya baadhi ya marubani wa hapa nchini wakati wa uzinduzi wa kozi ya wahudumu wa ndani ya ndege iliyozinduliwa jana
Katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam.

n4

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe wakatikati aliyekaa
kwenye viti akiwa katika picha ya wanafunzi wa kozi ya uhudumu ndani ya ndege, wakati wa uzinduzi wa kozi hiyo iliyozinduliwa jana  Katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam.

n5 n6

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe akizungumzawakati wa , wakati wa uzinduzi wa kozi hiyo iliyozinduliwa jana Katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam.

………………………………………………………………………………..

Katika kuhakikisha Nchi inakwenda na kauli mbiu ya hapa kazi tu na kuendanana na kasi ya Rais John Magufuli katika uwajibikaji hasa kwenye sekta ya Anga, Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimezindua Kozi ya wahudumu wa ndani ya ndege ili kuhakikisha uwekezaji wa ndege nchini unaendana na Rasilimali watu wenye ujuzi.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kozi hiyo uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha NIT jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isaac Kamwelwe amesema kuwa kuwepo kwa kozi hiyo, kutasaidia kupata wajuzi wazawa wengi na kuacha kutoa wahudumu wa ndege nje ya maji.

“Kozi hii itasaidia sana, sasa hatuwezi kutoa wahudumu wa ndege nje ya maji, na nitajujulisha hawa waliofundishwa wanafanya kazi ATCL”, nitasimamia hili ili kuhakikisha sekta ya afya itakuwa na insimu, hakuna kurudi nyuma tena, Amesema mhandisi Kamwele

Mhandisi Kamwelwe amesema upatikanaji wa rasilimali watu katika Sekta ya anga utasaidia sana kuhakikisha tunakuza uchumi wa ndani na kupunguza changamoto ya kutokuwepo kwa rasilimali Ambayo ilikuwa ukipelekea watu wengi kusoma nje ya nchi au kuhitajika kwa watu wa nje ya nchi ambao wanalipwa fedha nyingi.

Ameongeza kuwa uchumi wa viwanda unategemea zaidi, usafiri wa anga katika usafirishaji wa bidhaa katika masoko ya nje kwa haraka zaidi.

Amesema anaamini kuwa wataalamu mbalimbali wakiwemo wahandisi wa masuala ya ndege wanaofundishwa katika chuo cha NIT wanaujuzi wa kutosha wa kuweza kutengeneza ndege zetu sita ikiwemo inayoingia Léo nchini hivyo- amewataka kuhakiksha wanaitumia KIA kuonyesha ujuzi huo.

Aidha Ameongeza, serikali inaendelea kununua ndege hivyo wahudumu wa ndege hawawezi kuwatoa nje ya Tanzania bali itawaajiri wale wote waliopata mafunzo ya kozi hiyo katika chuo cha NIT.

Amesema lengo la kuboresha elimu inayotolewa katika chuo cha NIT, Serikali kupitia wizara yake imeshakamilisha mzungumzo ya kupata fedha kutoka Benki ya Dunia na Serikali ya China kwa ajili ya kuboresha miundombinu, kukarabati kalakana na ununuiz wa vifaa vya kufundishia katika chuo hicho.

Aidha Mhandisi Kamwelwea amewataka NIT kuendelea kubuni zaidi katika kuzalisha Rasilimali watu wa kuweza kuhudumia ndege zetu na kuacha kutegemea rasilimali inayotoka nje ya nchi.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha NIT Profesa Zakaria Mganilwa amesema kuwa wamejipanga katika uzalishaji wa
rasilimali watu katika Sekta ya anga ili kuendana na Uwekezaji wa ndege unaofanywa nchini.
Amesema wahudumu ndani ya Ndege ni muhimu sana ambao ndio waangalizi wa usalama wa abiria na mali zao.

About bukuku

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × five =