Friday , March 22 2019

Home / MCHANGANYIKO / NAIBU KATIBU MKUU-UTUMISHI AOMBA USHIRIKIANO KUTOKA KWA WATUMISHI WA OFISI YAKE ILI KUFIKIA MALENGO YA MHE. RAIS YA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

NAIBU KATIBU MKUU-UTUMISHI AOMBA USHIRIKIANO KUTOKA KWA WATUMISHI WA OFISI YAKE ILI KUFIKIA MALENGO YA MHE. RAIS YA KUTOA HUDUMA BORA KWA WANANCHI

IMG_2095

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Peter Mabale mara baada ya kuripoti  ofisini kwake  jijini  Dodoma leo kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

IMG_2115

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuripoti ofisini kwake leo jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

IMG_2128

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Bw. Donald Bombo, akimtambulisha Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael kwa menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, kabla ya Naibu Katibu Mkuu huyo kuzungumza na menejimenti leo jijini Dodoma.

IMG_2142

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akizungumza na menejimenti ya ofisi yake alipokutana nao leo jijini Dodoma kwa lengo kufahamiana ili kuanza kazi rasmi.

IMG_2146

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael akisisitiza jambo kwa wajumbe wa kikao cha menejimenti ya ofisi yake (hawapo pichani) alipokutana nao leo jijini Dodoma kwa lengo kufahamiana na kuanza kazi rasmi.

…………………

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Francis Michael ameomba kupewa ushirikiano na watumishi wa ofisi yake ili kuhakikisha huduma bora inatolewa kwa wadau na wananchi.

Dkt. Michael amesema hayo leo wakati akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora mara baada ya kuripoti ofisini kwake jijini Dodoma kwa ajili ya kuanza kazi rasmi.

Dkt. Michael amesema, watumishi wa ofisi yake wana uelewa mkubwa kuhusiana na masuala ya kiutumishi hivyo, ushirikiano atakaoupata utamsaidia kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kutimiza malengo ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya kuwahudumia wananchi.

Aidha, Dkt. Michael ameipongeza menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kuwahudumia watumishi wa umma nchini.

Dkt. Michael ameongeza kuwa, kazi ya kuwahudumia watumishi ni ngumu sana lakini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekuwa ikifanya vizuri sana na hii imejidhihirisha pale alipopata huduma inayostahili kupitia wawakilishi aliokuwa akiwaagiza mara kwa mara.

Dkt. Michael ameitaka menejimenti ya ofisi hiyo kuendelea kutoa ushirikiano kwake kama ilivyokuwa ikifanya kwa Naibu Katibu Mkuu aliyepita ili kufikia malengo ya Mheshimiwa Rais.

Naye, Mkurugenzi wa Idara ya TEHAMA Serikalini, Bw. Priscus Kiwango akitoa neno la shukrani kwa niaba ya menejimenti ya Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, ameahidi kutoa ushirikiano mzuri na kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kuwahudumia wananchi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.  Dkt. John Pombe Magufuli alimteua Dkt. Francis K. Michael kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, tarehe 08 Januari, 2019 na kumuapisha tarehe 09 Januari, 2019. Dkt. Michael amechukua nafasi ya Bi. Dorothy Mwaluko ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji).

 

About Alex

Check Also

PMO_0526

WAZIRI MKUU AZINDUA KIWANDA CHA KUCHAKATA MUHOGO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  na Mwenyekiti wa Kampuni ya Cassava Starch Of Tanzania Corporation Limited  (CSTC), Bw. Gerald …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eighteen − 6 =