Saturday , March 23 2019

Home / BURUDANI / TAMASHA LA PASAKA KUFANYIKA VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAMA APRILI 21/2019

TAMASHA LA PASAKA KUFANYIKA VIWANJA VYA POSTA KIJITONYAMA APRILI 21/2019

1

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo kuhusu maandalizi ya Tamasha la Pasaka.

2

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promosheni na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama akisisitiza jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari leo.

……………………………………………………………………………

Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion na muandaaji wa Tamasha la Pasaka Bw. Alex Msama amesema tamasha hilo mwaka huu litafanyika Aprili 21 kwenye viwanja vya Posta Kijitonyama jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Msama amesema viwanja vya posta ni mahali ambapo pako katikati zaidi na panaweza  kufikiwa na watu wa pande zote za jiji la Dar es salaam na ni eneo ambalo linafikika kirahisi .

Msama ameongeza kuwa mara baada ya tamasha hilo kufanyika jijini Dar es salaam litafanyika pia katika mikoa ya Dodoma, Mwanza, Simiyu na Iringa na wataongeza mikoa mingine kadiri ya mahitaji yatakavyokuwa ili kuhakikisha watu wote wanaopenda kupata burudani ya muziki wa injili kupitia Tamasha la Pasaka wanafikiwa.

Tamasha la Pasaka linatarajiwa kushirikisha  wanamuziki mbalimbali wa nchini Tanzania na nje ya Tanzania.

Msama amesema maandalizi ya tamasha hilo yanaendelea vizuri ambapo mpaka sasa tayari wamekamilisha mazungumzo na mwimbaji mmoja kutoka nje hata hivyo hakumtaja jina lake.

Awali Msama alisema wako katika mazungumza na wanamuziki kutoka Marekani, Uingereza , Afrika Kusini, Nigeria , Kenya na Tanzania pia.

About bukuku

Check Also

Picture 1

WASHINDI 15 WAPATIKANA PROMOSHENI YA TIA KITU PATA VITUZ NA DStv!

Mkuu wa Kitengo cha Thamani kwa wateja MultiChoice Tanzania Hilda Nakajumo akizungumza na waandishi wakati …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

17 − 9 =