Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / Mloganzila yapongezwa kuimarisha huduma kwa wananchi

Mloganzila yapongezwa kuimarisha huduma kwa wananchi

Bodi 01

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Charles Majinge (kulia) akizungumza katika kikao cha kawaida cha bodi hiyo kilichofanyika katika Hospitali ya Mloganzila ambapo Menejimenti iliwasilisha taarifa ya utendaji kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka, Oktoba hadi Desemba, 2018. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru.

Bodi 02

Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Wakurugenzi wa Hospitali hiyo wakimsikiliza Mwenyekiti wa bodi hiyo Prof. Charles Majinge alipokua akizungumza katika kikao hicho.

Bodi jpeg 03

Mjumbe wa bodi Dkt. Grace Magembe akichangia jambo katika kikao hicho kilichofanyika katika Hospitali ya Mloganzila.

Bodi jpeg 04

Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Andrea Pembe (kushoto) akizungumza katika kikao hicho, kulia ni Meya wa Jiji la Dar es salaam Mh. Isaya Mwita ambaye ni mmoja wa wajumbe wa bodi hiyo.

Bodi jpeg 05

Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi (wapili kushoto) akiwaelezea wajumbe wa bodi utoaji wa huduma katika hospitali hiyo. Wajumbe hao wamepata fursa ya kutembelea sehemu mbalimbali za kutolea huduma katika hospitali hiyo.

……………………………………………………………………………………..

Bodi ya Wadhamini, Hospitali ya Taifa Muhimbili imeupongeza Uongozi wa kwa kuboresha huduma za afya kwa wananchi katika Hospitali ya Mloganzila.

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini, Prof. Charles Majinge katika kikao cha kawaida cha Bodi hiyo kilichofanyika Hospitali ya Mloganzila ambapo Menejimenti iliwasilisha taarifa ya utendaji kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka cha Oktoba hadi Desemba, 2018.

Nafahamu kumekuwa na changamoto kadhaa katika Hospitali hii ya Mloganzila, lakini nafurahi kuona kila siku Menejimenti inavyotatua changamoto hizo na hivyo wananchi kuitikia wito wa kutumia huduma zinazopatikana hapa, aliema Prof. Majinge.

“Napenda kwa dhati kabisa mfahamu kuwa Bodi yangu tunaridhishwa sana na utendaji kazi wa Hospitali ya Mloganzila kwani hata malalamiko yaliyokuwa yakitolewa na wananchi kuhusu utoaji wa huduma yanaendelea kupungua siku hadi siku, hivyo hii ni hatua nzuri na ya kupongezwa”, alisema Prof. Majinge.

Sisi kama Bodi ya Wadhamini, tunaomba kila mmoja wenu atimize wajibu wake mahali pake pa kazi ili Mloganzila iwe moja ya hospitali bora hapa nchini katika kutoa huduma za kibingwa, kufundisha na kufanya tafiti, alisisitiza Prof. Majinge.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Lawrence Museru ambaye pia ndiye mwenye dhamana ya kusimamia Hospitali ya Mloganzila alisema pamoja na hospitali hiyo kukabiliwa na changamoto mbalimbali, Menejimenti imejipanga kuhakikisha inatoa huduma za kibingwa na za kibobezi kama ilivyokusudiwa.

Naye Kaimu, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila Dkt. Julieth Magandi amesema kumekuwa na ongezeko la wagonjwa katika kipindi cha robo ya pili ya mwaka ambapo wagonjwa wa nje 20,173 walihudumiwa ukilinganisha na wagonjwa 17,116 waliohudumiwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu sawa na ongezeko la asilimia 17.8.

Dkt. Magandi amesema upande wa wagonjwa waliolazwa kulikuwa na ongezeko la asilimia 29.6 kutoka wagonjwa 1,459 hadi 1,891, wakati upande wa huduma za upasuaji jumla ya wagonjwa 649 walifanyiwa upasuaji  ukilinganisha na upasuaji wa wagonjwa 267 katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa fedha ambalo ni ongezeko la  asilimia 143.

Kwa upande wa huduma za tiba shirikishi inayojumuisha maabara na huduma za radiolojia kulikuwa na ongezeko la huduma ambapo maabara ilipokea jumla ya sampuli za vipimo mbalimbali 28,907 kwa wagonjwa waliolazwa na wa nje ukilinganisha na sampuli 16,233 katika robo ya kwanza ya mwaka ikionesha ongezeko la sampuli 12,674 ni sawa na asilimia 78, alisema Dkt. Magandi.

Dkt. Magandi alisema katika huduma za radiolojia zinazojumuisha vipimo vya CT scan, MRI, X-ray n.k kulikuwa na ongezeko la vipimo asilimia 47 ambapo vipimo 5,221 vilipimwa katika kipindi hicho ukilinganisha na vipimo 3,541 na huduma katika maeneo yote ya Hospitali zinaendelea kuimarishwa siku hadi siku.

Oktoba 3, 2018 Serikali iliiweka Hospitali ya Taaluma na Tiba ya Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MAMC) Mloganzila chini ya Mamlaka ya Usimamizi na Uendeshaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).

MNH inasimamiwa na Mkurugenzi Mtendaji Prof. Lawrence Museru hivyo ili kuhakikisha shughuli za utoaji huduma zinaendelea kutekelezwa, Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Taifa Muhimbili katika kikao chake cha 18 kilichofanyika Oktoba 12, 2018 ilimteua Dkt. Julieth Magandi kuwa Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Mloganzila. Kutokana na uteuzi huo Dkt. Magandi anaripoti chini ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH ili kusimamia shughuli za kila siku za hospitali hiyo.

Kwa sasa MNH imeweka mikakati ya kuimarisha huduma mbalimbali zikiwemo huduma za kibingwa ili kutimiza majukumu yake kama ilivyokusudiwa. Hospitali hiyo ina vitanda 608.

Hospitali ya Mloganzila ni inatoa huduma za tiba za kibingwa na kibobezi, mafunzo na tafiti. Hospitali hiyo ilifunguliwa rasmi tarehe 25 Novemba 2017 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Joseph Pombe Magufuli.

About bukuku

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

three × 3 =