Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / WATUHUMIWA WATATU WA MAUAJI YA WATOTO 3 WA FAMILIA MOJA WAFIKISHWA KORTIN NJOMBE

WATUHUMIWA WATATU WA MAUAJI YA WATOTO 3 WA FAMILIA MOJA WAFIKISHWA KORTIN NJOMBE

unnamed
NJOMBE 
Kesi dhidi ya jamhuri na watuhumiwa watatu wa mauaji ya watoto watatu wa familia moja yalifanyika january 20 katika kijiji cha Ikando kata ya kichiwa wilayani Njombe imetajwa leo kwa mara ya kwanza katika mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Njombe na kuahirishwa itakaposomwa tena mpaka 25 februari.
Kesi hiyo ambayo imesomwa kwa mara ya kwanza katika mahakama hiyo na Hakimu mkazi Magdalena Ntandu imewataja watuhumiwa watatu akiwemo Jeol Nziku(35),Nasson Kaduma(39) na Alphonce Edward(51) kuhusika na mauaji ya watoto hao watatu wanaojulikana kwa majina ya Gasper Nziku, Giliard Nziku na Godwin Nziku ambayo yalitekelezwa januari 20 katika kijiji cha Ikando.
Akisoma mashtaka kwa watuhumiwa Ntandu amesema watuhumiwa wanatuhumiwa kwa mashtaka matatu ya mauaji na kudai kwamba Watuhumiwa wanarudishwa mahabusu mpaka februari 25 kesi itakapotajwa tena  huku pia akidai watuhumiwa watafikishwa mahakama kuu kujibu mashtaka yanayowakabili pindi tu upelelezi utakapo kamilika.
Kufikishwa mahakamani kwa watuhumiwa watatu pekee kati ya 30 walioripotiwa kukamatwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhusika na utekaji na mauaji ya watoto wilayani Njombe kunaibua maswali kwa waandishi wa habari na kumtafuta mkuu wa operesheni maalumu Tanzania Kamanda Liberat Sabas ambaye anadai jeshi linaendelea na upelelezi kwa watuhumiwa wengine pna kwamba pindi utakapokamilika watafikishwa mahakamani huku akitoa onyo juu ya migogoro ya kifamilia na imani za kishirikina.
Ahmed Seif  pamoja na Yohana Misango ni mawakili wanaosimamia kesi hiyo dhidi ya jamhuri na watuhumiwa hao watatu
wa mauaji.

About Alex

Check Also

_MG_1453

ASKARI WA JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI MIKOA YA KANDA YA KASKAZINI WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA WALEDI

 Mwenyekiti wa kikao kazi ,Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Arusha Mrakibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

twelve − eleven =