Saturday , March 23 2019

Home / MICHEZO / SERENGETI BOYS KAMBINI ARUSHA

SERENGETI BOYS KAMBINI ARUSHA

csHohjF-_400x400
Timu ya Taifa ya Vijana U17 “Serengeti Boys” imepiga Kambi Jijini Arusha kujiandaa na Fainali za Afrika za Vijana U17 zitakazofanyika Tanzania mwezi Aprili.
Serengeti Boys inaendelea na maandalizi katika Uwanja wa Aghakhan mazoezi yakifanyika asubuhi na jioni.
Itarudi Dar es salaam mwishoni mwa mwezi Februari kabla ya kuondoka Machi 1,2019 kueleka nchini Uturuki kwenye mashindano ya UEFA ASSIST yanayoshirikisha timu 8 za Afrika na timu 4 za Ulaya zilizogawanywa kwenye makundi 3.
Wachezi 31 wapo Kambini Jijini Arusha wakiendelea na mazoezi hayo kujiandaa na AFCON U17 itakayofanyika Tanzania.
Tayari nembo ya mashindano hayo imezinduliwa wakati vikao mbalimbali vya Kamati ya maandalizi vikiendelea.

About Alex

Check Also

PIX 4

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Yaridhishwa na Upanuzi wa Usikivu wa TBC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Ryoba(mwenye tai nyekundu) akiwasilisha Taarifa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five × 1 =