Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / TBL Yang’ara Viwanda vya kutengeneza Bia Barani Afrika

TBL Yang’ara Viwanda vya kutengeneza Bia Barani Afrika

PICHA TUZO

Maofisa wa viwanda vya ABInBev wakiwa wameshikilia vyeti vya tuzo walivyojishindia katika  hafla ya kutunuku tuzo hizo nchini Afrika ya Kusini

………………………..

-Yazoa tuzo mbalimbali za viwango vya ubora na usalama

kampuni ya TBL imeshinda tuzo mbalimbali za kimataifa na kiwanda cha Mbeya kushikilia nafasi ya pili kwa ubora barani Afrika baada ya kushindanishwa na viwanda  vilivyopo chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBev katika mataifa mbalimbali duniani.

Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilifanyika nchini Afrika ya kusini na kuhudhuriwa na viongozi waandamizi wa kampuni hiyo na baadhi ya wafanyakazi kutoka sehemu mbalimbali ambapo inaendeshea biashara zake.

Viwanda hivyo vya bia vilivyopo katika mikoa ya Mbeya, Dar es Salaam, Mwanza na Arusha vimeshinda tuzo za nyanja mbalimbali ikiwemo kuzingatia usalama, uzalishaji wa viwango vya kimataifa na   kuzingatia matumizi ya ufanisi ya mfumo wa uzalishaji unaotumiwa na makampuni ya ABInBev ujulikanao kama Voyage Plant Optimization Conference (VPO). Pia bia ya Safari (Dar Es Salaam na Kilimanjaro (Mbeya) zimeibuka kidedea kwa ubora.

Akiongelea mafanikio haya, Meneja Mawasiliano wa TBL, Abigail Mutaboyerwa, alisema kampuni inajivunia rekodi ya ushindi inayowekwa na viwanda vyake nchini na ni uthibitisho halisi kuwa watanzania tunaweza kufanya vizuri na kuleta maendeleo kwa kasi tukiamua kujituma na kufanya kazi kwa bidii.

Alisema ushindi huu unatokana na jitihada za pamoja kutoka kwa wafanyakazi wote wa kampuni ambao wanafanya kazi kwa bidii na weredi mkubwa kwa kutumia mifumo ya kimataifa ya uendeshaji wa viwanda na kuhakikisha mafanikio haya yanapatikana na kuongeza kuwa kampuni itaendelea kuunga mkono jitohada za serikali ya awamu ya tano za kuleta mapinduzi katika sekta ya viwanda nchini.

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × three =