Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / MTAMBO WA KUCHAKATA ASALI WAFUNGWA WILAYANI MANYONI

MTAMBO WA KUCHAKATA ASALI WAFUNGWA WILAYANI MANYONI

index

Mtendaji Mkuu wa TFS Profesa Dos Sontos Silayo akiangalia mitambo ya kuchakata asali iliyofungwa wilayani Manyoni mkoani Singida

A

Mitambo ya kuchakata asali ambayo imefungwa katika kiwanda cha TFS wilayani Manyoni,mkoani Singida

……………………..

Mwandishi wetu

WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) umefunga mtambo wa kuchakata asali wilayani Manyoni mkoani Singida.

Akizungumza leo Machi 14,2019 Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano TFS Tulizo Kilaga amesema mtambo  huo wa kisasa una uwezo wa kuchakata lita 500 kwa siku.

 

 

Amesema kuwa mtambo huo umegharimu Sh.milioni 80 na unatarajiwa kuondoa changamoto ya uwepo wa asali yenye kiwango duni cha ubora katika ukanda huo na maeneo maeneo ya jirani.

“Mtambo huu umefungwa katika kiwanda cha TFS na utatumiwa na wafugaji wa nyuki wa ndani pamoja na nje wote wataruhusiwa kuchakata mazao yao,”amesema Kilaga.

Ameongeza kuwa kiwanda hiko kwa kiasi kikubwa kitategemea mali ghafi toka kwenye msitu wa Aghondi uliopo eneo la Itigi na uwepo

wa mtambo huo pia utasaidia kutunza mazingira kwani watakuwa na uhakika wa soko la asali yao.

Pia amesema katika uvunaji wa awali wamefanikiwa kuvuna mizinga 459 kati ya 729 na kupata asali kilo  6,175 sawa na tani 6.175 wastani kilo 13.45 kwa mzinga.

Akizungumzia mtambo huo, Meneja wa TFS wilayani Manyoni Juma Mambo amesema utasaidia kupatikana kwa asali bora na hivyo kuwa na uhakika wa soko la ndani na nje ambalo litawafanya wadau kujiongezea kipato.

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

sixteen + 3 =