Saturday , March 23 2019

Home / BURUDANI / TAMTHILIYA MPYA YA WAARIS KUONYESHWA KWENYE STARTIMES SWAHILI

TAMTHILIYA MPYA YA WAARIS KUONYESHWA KWENYE STARTIMES SWAHILI

GY3A09120

Meneja masoko wa Startimes Davis Malisa  akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kuonesha tamthiliya mpya ya kihindi iliyotafasiriwa na kuingiziwa sauti za Kiswahili itakayokuwa inaoneshwa kupitia kwenye kingamuzi cha Startimes leo uliofanyika katika ukumbi wa sinema uliopo mlimani City jijini Dar es Salaam.
…………….

Dar es salaam,

Kampuni ya Star Media (T) Ltd leo imetangaza ujio wa tamthiliya mpya ya kihindi iliyotafasiriwa na kuingiziwa sauti za Kiswahili hapa hapa nchini. Tamthiliya ya Waaris ama kwa jina la Kiswahili Mrithi inakuwa ni tamthiliya ya kwanza kwenye king’amuzi cha StarTimes iliyoingizwa sauti za Kiswahili hapa hapa Tanzania.

Katika kuhakikisha wateja wao wanapata burudani wanayostahili, StarTimes kupitia chaneli ya ST Swahili wataanza kuonyesha tamthiliya hiyo siku ya Alhamisi tarehe 14 Machi mwaka huu.

“Tunaendelea kujipambanua kama wafalme wa Burudani za kifamilia, na tamthiliya hii mpya ni aina ya maudhui ambayo yanaweza kuangaliwa na familia nzima. Tamthiliya ya Waaris ama kwa Kiswahili Mrithi itaanza kuonekana kwenye chaneli yetu ya StarTimes Swahili siku za Alhamisi na Ijumaa kuanzia saa 2:30 hadi saa 3:30 Usiku.” David Malisa, Meneja Masoko StarTimes Tanzania.

“Waaris inazungumzia maisha ya mwanamke, Amba Pawaniya mama wa kihindi ambaye analizimika kumlea mtoto wake wa kike, Manpreet Pawaniya, kama wa kiume katika jitihada za kulinda amani kijijini kwao na kumzuia shemeji yake Jaggan Pawaniya ambaye ni mkorofi asishike madaraka.

“Tamthiliya inaonyesha matokeo ya malezi hayo na mambo mengine. Pia inaonyesha unyanyasaji wa kijinsia ambao pia bado ni changamoto katika jamii zetu, bila kusahau uhalisia wa ambavyo kina mama wanawalinda watoto wao.” David Malisa akizungumzia simulizi ya tamthiliya ya Waaris.

Miongoni mwa wasanii walioshiriki kuingiza sauti za Kiswahili katika tamthiliya ya Waaris ni Vyonne Cherry (Monalisa), Godliver Gordian, Sophie na Rakheem David ambao wana uwezo wa hali ya juu katika kuingiza sauti na kwa ujumla wameitendea haki Waaris.

Tamthiliya ya Waaris itaonyeshwa na chaneli ya ST Swahili pekee ambayo inapatikana katika kifurushi cha Nyota kwa Tsh 8000 kwa watumiaji wa Antenna na Tsh 11,000 kwa watumiaji wa dikoda za Antenna.

 

Kuhusu Star Media (T) Ltd

StarTimes ni kampuni ya Matangazo ya kidigitali inayoongoza Africa, ikihudumia zaidi ya wateja milioni 10 katika bara zima. StarTimes inamiliki jukwaa la maudhui lenye chaneli 480 zikiwemo chaneli za Habari, filamu, tamthiliya, michezo, burudani, vipindi vya watoto, mitindo, dini na vingine vingi. Matazamio ya Kampuni ni “Kuhakikisha kila familia ya kiafrika inapata, inamudu, inatazama na kushiriki kwenye Uzuri wa Televisheni ya kidigitali”

Tembelea tovuti yetu: www.startimestz.com

About Alex

Check Also

5

WASOMI NCHINI KUANDIKA HISTORIA UPYA HISTORIA YA UKOMBOZI WA TANZANIA

Nyumba ambayo wanaharakati wa kudai Uhuru nchini kutoka Wilayani Urambo walikuwa wakiendeshea vikao vyao vya …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

five − two =