Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / UFAHAMU MDOGO CHANZO CHA UKEKETAJI

UFAHAMU MDOGO CHANZO CHA UKEKETAJI

Pix 1

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bw. Atupele Mwambene akizungumza na wadau wa kupinga ukeketaji nchini wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau hao jijini Dodoma kujadili Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukeketaji.

Pix 2

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bi. Mwajuma Magwiza akieleza mchakato wa kuandaa Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukeketaji kwa wadau wa kupinga ukeketaji nchini wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau hao jijini Dodoma kujadili Mkakati huo.

Pix 3

Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bi. Tausi Mwilima akielezea jambo kwa wadau wa kupinga ukeketaji nchini wakati wa kikao kazi kilichowakutanisha wadau hao jijini Dodoma kujadili Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukeketaji.

Pix 4

Mshauri Mwelekezi kutoka Shirika la Hodari TZ Bi. Imelda Urrio akifafanua baadhi ya mambo kuhusu Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukeketaji nchini wakati wa kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kilichowakutanisha wadau wa kupinga Ukeketaji nchini.

Pix 5

Baadhi ya wadau wa lupinga ukeketaji wakifuatilia mada mablimbali zilizkuwa zikitolewa katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma kilichokutanisha wadau hao kujadili Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukeketaji nchini.

Pix 6

Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bw. Atupele Mwambene (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wakupinga ukeketaji nchini mara baada ya kikao kazi kilichowakutanisha kujadili kuhusu Mkakati wa Kitaifa wa Kutokomeza Ukeketaji nchini kilichofanyika jijini Dodoma.

Picha Kitengo cha Mawasiliano -WAMJW

…………………..

Na Mwandishi Wetu Dodoma

Inaelezwa kuwa ufahamu mdogo wa madhara ya ukeketaji miongoni mwa jamii, wazazi na walezi ni moja ya sababu ya kuendelea kwa vitendo hivyo pamoja na jitihada mbalimbali za Serikali na wadau katika kuhakikisha ukeketaji unatokomezwa katika katika jamii za kitanzania.

 Hayo yamebainika leo jijini Dodoma wakati wa kikao kazi kilichokutanisha Maafisa Maendeleo yanJamii na Ustawi wa Jamii kutoka katika mikoa kumi inayoongoza kwa ukeketaji nchini kilichoandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na  Shirika la Amref Tanzania.

Akizungumza katika kikao hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bw. Atupele Mwambene amesema kuwa ukeketaji ni mojawapo ya mila na desturi zenye madhara zinazofanyika katika baadhi ya jamii hapa nchini na mwanzo mila hizo zilikuwa zikifanyika kwa wasichana wa rika la kuolewa ila kwasasa vitendo hivyo vinafanyika hata kwa watoto wachanga na kwa watu wazima wakati wakujifungua.

Ameongeza kuwa Mila na desturi hizo zenye madhara zinakwamisha jitihada za wananchi kushiriki katika kujiletea maendeleo lakini pia kushiriki katika kuchangia kujenga na kukuza uchumi wa taifa.

Bw. Mwambene amebainisha kuwa kulingana na Takwimu za Taarifa ya Utafiti wa Afya ya mama na Mtoto na viashiria vya Malaria ya Mwaka 2015/16 inaonesha kwamba mikoa kumi inayooongoza kwa ukeketaji ni Manyara asilimia (58), Dodoma (47), Arusha (41) Mara (32), Singida (31), Tanga (14), Kilimanjaro (10), Morogoro (9), Iringa (8) na Njombe (7).

“Hii inamaanisha kuwa tatizo la ukeketaji kwa wanawake na watoto bado linaendelea na hivyo jitihada za makusudi zinahitajika katika kukabiliana nalo hivyo mkakati wa kupambana na ukeketaji ni nyenzo muhimu, madhubuti katika kukabiliana na tatizo hili” alisema

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Idara ya Maendeleo ya Mtoto kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Idara Kuu Maendeleo ya Jamii) Bi. Mwajuma Magwiza amesema kuwa mchakato wa kuandaa mkakati huo ulianza mwaka 2017 mwezi Agosti kwa kufanya majadiliano na wadau kwa kuangalia namna ya kufikia lengo la kupunguza ukeketaji kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2022.

Ameongeza kuwa kwa mujibu wa Takwimu za Taarifa ya Utafiti wa Afya ya Uzazi na mtoto na viashiria vya Malaria nchini ya mwaka 2015/16 zinaonesha kwamba kitaifa hali ya ukeketaji imeshuka kutoka asilimia 18 mwaka 2010 hadi asilimia 10 mwaka 2015/16 ingawa kuna baadhi ya mikoa bado takwimu ziko juu.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Manyara Bi. Fisso amesema kuwa Makakti huo utasaidia kuondokana na vitendo vya ukeketaji kwa kuwekeza katika kuwapa elimu watoto katika shule za Msingi na Sekondari ili waweze kutoa taarifa ya vitendo hivyo kwani kwasasa vimekuwa vikifanywa kwa watoto zaidi.

Pia Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka mkoa wa Mara Bi. Frolida Magori ameeleza kuwa Mkakati huo wa kutokomeza ukeketaji nchini utakuwa ni chachu ya kuleta mabadiliko kwa kutoa elimu kwa jamii hasa ya mkoa wa Mara kuondokana na Mila na Desturi zenye madahara ambazo zinapelekea kuwepo kwa vitendo hivyo.

Serikali na Wadau wamekutana kujadili Mkakati wa Kitaifa wa kutokomeza ukekektaji dhidi ya watoto na Wanawake nchini ikiwa na lengo la kuhakikisha mkakati huu unakuwa nyenzo muhimu katika utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kupambana na Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto                ( MTAKUWWA).

 

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × two =