Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / WADAU WA NISHATI WAPANGA KUTATUA TATIZO LA UMEME

WADAU WA NISHATI WAPANGA KUTATUA TATIZO LA UMEME

IMG-20190314-WA0056
Wadau wa Nishati kutoka sehemu mbalimbali wakifuatilia mjadala wa kutatua mapungufu yaliopo katika sekta ya Nishati. 
IMG-20190314-WA0039
Kaimu Kamishina Msaidizi wa nishati jadidifu wizara ya Nishati Edward Leornad Ishengoma akiendesha mkutano. 
………………………
Na Emmanuel Mbatilo
Wadau wa nishati kutoka katika nchi mbalimbali kushirikiana na Wizara ya Nishati hapa nchini wamekutana kwa ajili ya kupanga mikakati thabiti ambayo itasaidia kukuza sekta ya Nishati ili kufikia uchumi wa Kati wa Viwanda. 
Akizungumza na wadau mbalimbali jijini Dar es Salaam, Kaimu Kamishina msaidizi wa nishati jadidifu Edward Ishengoma amesema lengo la kukutana na wadau ni pamoja na kuwaweka wadau hao pamoja na kuangalia namna gani wanaweza kutatua changamoto ambazo zinaikabili Sekta ya Nishati.
Aidha, Ishengoma amesema kuwa, uboreshaji katika sekta ya nishati itasaidia kuongeza uzalishaji tuwe na umeme wa kutosha kuweza kuendesha viwanda.
 “Kuondoa vikwazo na kuendeleza Sekta ya Nishati ili iweze kuchangia kikamilifu kwenye kuongeza uchumi wa taifa pamoja na nchi nyingine”. Amesema Ishengoma

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

eleven − 5 =