Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / WATOTO NJITI HATARINI HOSPITALI YA RUFAA NJOMBE

WATOTO NJITI HATARINI HOSPITALI YA RUFAA NJOMBE

vlcsnap-2019-03-14-05h39m27s240.png

NJOMBE 
Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Njombe Kibena imekiri kukabiliwa na changamoto ya chumba cha kuhifadhia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati(NJITI) hatua ambayo inailazimu hospitali hiyo wakati mwigine kuhifadhi watoto zaidi  ya  20 katika chumba kimoja kilichopo chenye uwezo wa kubeba watoto wanne.
Kutokana na hali hiyo serikali mkoani humo imelazimika kuanza mpango wa ujenzi wa jengo la kisasa la kuhifadhia watoto hao hospiali hapo litakalogharimu zaidi mil 80 huku ikitoa rai kwa wadau wa maendeleo pamoja na mwananchi anaeguswa na changamoto hiyo kuchangia ujenzi huo.
Joseph Kimaro ambay ni kaimu mganga hospitali ya rufaa Kibena na Erica Balama daktari mbobezi wa watoto wanasema mrundikano wa watoto katika kitanda kimoja na huku wakilazimika kuhifadhi watoto zaidi ya 20 katika chumba chenye uwezo wa kuhifadhi watoto wanne inahatarisha usalama wa watoto hao kiafya na kudai kwamba ilikutatua changamoto hiyo tayari mchakato wa ujenzi wa jengo la kisasa umeanza huku wadau na wananchi wapenda maendeleo wkiombwa kuchangia kufanikisha zoezi hilo.
Baada ya serikali kupitia ongozi wa hospitali kuweka bayana changamoto hiyo Jonson Mgimba ambaye ni katibu wa hamasa na chipukizi UVCCM mkoa wa Njombe na Sadoki Mwanda wanaguswa na hali hiyo na kuamua kuchangia mifuko ya saruji 70 yenye thamani ya zaidi ya laki 7 .
Mtandao huu uimezungumza baadhi ya akina mama waliofanikiwa kujifungua watoto NJITI akiwemo Witnes Nyatto na Oria Mwalongo ambaye amejifungua mapacha  ambao wanaelezea changamoto hiyo huku wakiomba serikali kuongeza jengo .
Kwa takwimu za 2018 hospitali ya Rufaa Kibena imepata watoto njiti 446 huku themanini wakidaiwa kufariki dunia.
 

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

11 − 3 =