Saturday , March 23 2019

Home / MICHEZO / ARSENAL YAPEWA NAPOLI ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

ARSENAL YAPEWA NAPOLI ROBO FAINALI EUROPA LEAGUE

Arsenal itamenyana na Napoli, Chelsea na Slavia Prague katika Robo Fainali ya Europa League

 EUROPA LEAGUE DRAW

QUARTER-FINAL DRAW
Napoli vs Arsenal
Villarreal vs Valencia
Benfica vs Frankfurt
Slavia Prague vs Chelsea
 
 
 
SEMI-FINAL DRAW 
Napoli/Arsenal vs Villarreal/Valencia
Benfica/Frankfurt vs Slavia Prague/Chelsea
 
 

TIMU ya Arsenal ya England itamenyana na Napoli katika Robo Fainali ya Europa League. 
Katika droo iliyopangwa leo mjini Nyon, Uswisi, kikosi cha Maurizio Sarri, Chelsea ambayo haijapoteza mechi hadi sasa kwenye mashindano haya, yenyewe itamenyana na Slavia Prague.
Kutakuwa na mtanange wa timu za Hispania tupu kati ya Villarreal na Valencia wakati Benfica itamenyana na Frankfurt katika kuwania Nusu Fainali.

Mechi za kwanza zitachezwa Aprili 11 na marudiano Aprili 18.
Chelsea itaanzia nyumbani kwa sababu zote, The Blues na Arsenal haziwezi kucheza London katika usiku mmoja. 
Mshindi wa mechi kati ya Chelsea na Slavia Prague atakutana na mshindi wa mechi kati ya Frankfurt na Benfica. 
Arsenal wameshinda nyumbani tu katika mechi zao zilizopita dhidi ya Napoli kwenye michuano ya Ulaya, wakati walipowafunga wababe hao wa Serie A 2-0 kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2013-14, Mesut Ozil akihusika katika mabao yote.
Mjerumani huyo alifunga na kutoa pasi ya bao lingine kwenye mechi hiyo Uwanja wa Emirates. 

About Alex

Check Also

PIX 4

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Yaridhishwa na Upanuzi wa Usikivu wa TBC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Ryoba(mwenye tai nyekundu) akiwasilisha Taarifa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

8 + three =