Saturday , March 23 2019

Home / MICHEZO / MAN UNITED USO KWA USO NA MIAMBA YA HISPANIA BARCELONA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

MAN UNITED USO KWA USO NA MIAMBA YA HISPANIA BARCELONA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

TIMU ya Manchester City itamenyana na Tottenham Hotspur katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika droo iliyopangwa leo mjini Nyon, Uswisi, Manchester United watamenyana na Barcelona, wakati Liverpool itamenyana na FC Porto. 
Robo fainali nyingine itaikutanisha Ajax na Juventus na mechi za kwanza zitachezwa Aprili 9 na 10, wakati za marudiano zitafanyika Aprili 16 na 17.

ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA ULAYA 

Ajax vs Juventus
Liverpool vs Porto
Tottenham vs Manchester City
Barcelona vs Manchester United
Mechi za kwanza zitachezwa Aprili 9 na 10, na marudiano yatakuwa Aprili 16 na 17. 
NUSU-FINAL 
Tottenham/Man City vs Ajax/Juventus
Barcelona/Man United vs Liverpool/Porto
 

 

United itacheza mechi ya kwanza Uwanja wa nyumbani, Old Trafford kwa sababu wao na City hawawezi kucheza usiku mmoja mjini Manchester. 
Mshindi wa Robo Fainali ya timu za England tupu, Spurs na Man City atamenyana na mshindi kati ya Ajax na Juventus katika Nusu Fainali.
Wakati huo huo, Manchester United wanaweza kukutana na mahasimu wao wakubwa, Liverpool katika Nusu Fainali. 
Huku timu nne za Ligi Kuu England zikiwa zimetinga Robo Fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009, uwezekano wa mbili kati ya hizo kukutana ni mkubwa.
Vinara wa Ligi, City watalazimika kuwatupa nje wasumbufu Spurs ili kuweka hai matumaini ya kubeba taji la Ligi ya Mabingwa. 
City iliifunga Spurs 1-0 Uwanja wa Wembley kwenye mechi ya ligi mwezi Oktoba na timu hizo mbili zinatarajiwa kukutana wikiendi ya baada ya mechi ya marudiano. 
United ya kocha Ole Gunnar Solskjaer, iliyopindua matokeo dhidi ya Paris Saint-Germain kutoka kufungwa 2-0 nyumbani na kushinda 3-0 Hatua ya 16 Bora, inatakiwa kukiangusha kigogo kingine Ulaya, Barcelona.
Itakuwa ni marudio fainali za Ligi ya Mabingwa mwaka 2009 na 2011, ambazo zote Barcelona ilishinda, kikosi kikiwa chini ya kocha maarufu, Sir Alex Ferguson.

About Alex

Check Also

PIX 4

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii Yaridhishwa na Upanuzi wa Usikivu wa TBC

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC) Dkt.Ayoub Ryoba(mwenye tai nyekundu) akiwasilisha Taarifa …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × one =