Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / MHE BASHUNGWA AZINDUA TEKNOLOJIA ZA KILIMO HIFADHI SHADIDI ENDELEVU KWENYE MSETO WA MAZAO YA MAHINDI NA MIKUNDE

MHE BASHUNGWA AZINDUA TEKNOLOJIA ZA KILIMO HIFADHI SHADIDI ENDELEVU KWENYE MSETO WA MAZAO YA MAHINDI NA MIKUNDE

 

 

 

 

 
                       
Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo
 
Pamoja na umuhimu wa mazao Mseto ya Mahindi na Mikunde kwa usalama wa chakula na
kipato kwa wananchi, lakini uzalishaji wa mahindi bado ni mdogo , yaani wastani
wa gunia 5 za mahindi kwa ekari, na gunia 1 mpaka 2 za mbaazi au maharagwe
zenye uzito wa kilo mia mia kwa ekari katika mfumo wa kilimo mseto wa mazao
hayo.
 
Mavuno hayo madogo yanachangiwa kwa kiasi kikubwa
na mabadiiko ya tabia nchi, uhamishaji (mining)
wa rutuba ya udongo kwa miaka mingi, mmomonyoko wa udongo, kutokutumia mbegu
bora zinazostahimili mvua chache, kutokuzingatia kanuni za kilimo bora, ukosefu
wa ardhi kushindwa kuhifadhi unyevu kwa muda mrefu, magonjwa na visumbufu vya
mimea na kutokuwepo na masoko ya uhakika.
 
Hayo
yamebainishwa na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Innocent Bashungwa (Mb) wakati wa
uzinduzi wa teknolojia za kilimo
hifadhi shadidi endelevu kwenye mseto wa mazao ya mahindi na mikunde
katika
ukumbi wa Hoteli ya Mount Meru, Jijini Arusha jana tarehe 13 machi 2019.
 
Bashungwa alisema kuwa lengo kuu la Mradi huo wa SIMLESA
ni kuwasaidia wakulima kuzalisha zaidi na hivyo kuwa na uhakika wa chakula,
lishe bora, kuongeza kipato ili kuondokana na umaskini pamoja na kuzingatia
hifadhi ya ardhi na mazingira ambapo u
tekelezaji wake uliambatana pia na matumizi ya
mbinu za kilimo hifadhi.
 
Lengo lingine la mkutano huu ni kuwakutanisha wadau wa kutoka sekta za umma
na binafsi pamoja na wadau wa maendeleo ili kujadili na kupanga mikakati ya
kusambaza teknolojia ya kilimo hifadhi shadidi endelevu kwa wakulima wengi
katika maeneo mengi ili waweze kuongeza uzalishaji, uhakika wa chakula na
kipato na hatimaye kuboresha maisha yao.
 
Sambamba na hayo, Bashungwa
alisema kuwa Mradi wa SIMLESA umetekelezwa kwa kushirikiana na wadau hususani wakulima
na maafisa ugani. Katika jitihada hizo, Mradi umegundua teknolojia ya Kilimo
Hifadhi Shadidi Endelevu (CASI) katika mseto
wa mahindi na mikunde.
CASI
imethibitisha kuwa ni teknolojia inayoongeza tija, inaokoa muda (save time),
inaboresha hali ya afya ya udongo, ni teknolojia rafiki na ni njia ya
kukabiliana (coping) na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi.
 
“Pamoja na mafanikio hayo, katika
mazingira ya sasa na tukizingatia sera ya Serikali yetu ya Awamu ya Tano inavyotilia
mkazo Ujenzi wa uchumi wa viwanda ili kufikia uchumi wa kati, kuna umuhimu
mkubwa wa kushirikisha wabia mbalimbali katika kusambaza teknolojia hizo ili
manufaa yake yaweze kuwafikia idadi kubwa ya wanufaikaji hasa wakulima wetu”
Alikaririwa Mhe Bashungwa
 
 

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nineteen + twelve =