Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / MLOGANZILA YAPATIWA MSAADA WA VIFAA TIBA

MLOGANZILA YAPATIWA MSAADA WA VIFAA TIBA

001

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Prof. Lawrence Museru, (wa pili kutoka kushoto) akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Prof Sang Lyun Nam, (kulia) ni Prof. Seung –Kon Huh wa Korea Kusini. kushoto ni Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mloganzila Dkt. Julieth Magandi akishuhudia makabidhiano hayo.

OO2

Prof Lawrence Museru (wapili kutoka kushoto) akitoa neno la shukrani baada ya kupokea vifaa tiba ambavyo vitatumika katika vyumba vya upasuaji kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.

003

Pichani ni vifaa tiba Caiman Lerrafuse HF Generator (GN 200) pamoja na Infovac therapy system ambavyo vimetolewa leo katika Hospitali ya Mloganzila.

………………………

Dar es salaam                                                              

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila leo imepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 15 ambavyo vitatumika katika vyumba vya upasuaji kwa ajili ya kuwahudumia wagonjwa wenye vidonda.

Vifaa hivyo Caiman Lerrafuse HF Generator (GN 200) pamoja na Infovac Therapy System vimetolewa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya kina mama Prof. Sang Lyun Nam akiwa na Daktari Bingwa wa upasuaji ubongo na mishipa ya fahamu Prof. Seung -Kon Huh kutoka Korea Kusini.

Mkurugenzi Mtendaji wa MNH Prof. Lawrence Museru amesema vifaa hivyo vitasaidia utendaji kazi katika vyumba vya upasuaji, na kuongeza kuwa watalaam hao mbali na kutoa vifaa hivyo lakini pia wanafanya kazi na watalaam wa Hospitali ya Mloganzila hatua ambayo inasaidia wataalam wa hospitali hiyo kupata ujuzi zaidi.

“Wataalam hawa tupo nao hapa Mloganzila na wapo tayari kufundisha watanzania kufanya upasuaji ambao hatufanyi, hata msaada huu waliotupatia ni jitihada zao wenyewe, hivyo napenda kutumia fursa hii kuwashukuru sana kwa msaada huu wa vifaa tiba ambavyo tutatumia ipasavyo kama ilivyokusudiwa”. Amesema Prof. Museru.

Aidha Mkurugenzi huyo Mtendaji wa MNH amesema wanakamilisha mipango ya kuomba watalaam kutoka Korea ili waje kufanya kazi kwa muda na wataalam wa Muhimbili kwa lengo la kuwajengea uwezo katika maeneo mbalimbali ili kuendelea kutoa huduma bora na za kibingwa.

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

5 × two =