Saturday , March 23 2019

Home / BIASHARA / SERIKALI WALIOPEWA VIWANDA NA SERIKALI AMBAO HAWAJAVIENDELEZA KUNYANG’ANYWA

SERIKALI WALIOPEWA VIWANDA NA SERIKALI AMBAO HAWAJAVIENDELEZA KUNYANG’ANYWA

1H7A2060

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Naibu waziri wa viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya Amewataka waliopewa viwanda  wakati vilipo binafsishwa na hawajaviendeleza serikali itawanyang’anya mara moja bila kusita.

Akiongea wakati mbele ya kamati ya kudumu ya Bunge viwanda biashara na mazingira ilipotembelea kiwanda cha bia TBL mkoani hapa na shirika la utafiti wa zana za kilimo (CAMARTEC) mhandisi Manyanya amesema wapo waliopewa viwanda kwa nia nzuri ya kuviendeleza lakini hawajafanya hivyo na serikali itachukuwa hatua mara moja ya kuwanyang’anya.

Amesema kuwa msingi wa viwanda hivyo ni kuona vikiendelezwa na waliopewa kuweza kufikia uchumi wa kati wa viwanda ambapo akawataka kampuni ya bia TBL kuona umuhimu wa kuweka kiwanda mkoani Dodoma ili kuongeza tija ya uzalishaji wa bia nchini.

“Ni wasihi sana wale wote ambao wamepewa viwanda vilivyokuwa vya serikali wakati wa ubinafsishaji wakaviendeleza kabla serikali haijachukuwa hatua za kuwanyang’anya mara moja na pia ndugu zangu TBL fursa ya kuongeza wigo wa uzalishaji naomba mjenge kiwanda mkoani Dodoma”

Awali akiwasilisha mada mbele ya kamati hiyo Meneja wa kanda ya kaskazini wa kampuni ya bia TBL James Bokelo alisema kuwa kiwanda hicho kimekuwa na changamoto ya ufinyu wa eneo na pembeni yake kuna kiwanda ambacho kwa sasa hakifanyi kazi na kuiomba kamati kuishauri serikali ili waweze kuepewa eneo hilo kuongeza wigo wa uzalishaji na masoko yao kuliko sasa wakitegemea usafirishaji wa bia kutoka viwanda vingine kufidia pengo la uzalishaji.

Amesema kiwanda hicho kunakumbana na changamoto ya bei kubwa za maji na umeme pamoja na kodi ya huduma(Service Levy) ambapo pia awali kabla ya kutoa mabango yao kwenye jiji la Arusha walikuwa wakilipia million 600 kwa mwaka hivyo halmashauri kwa sasa imekuwa ikipoteza mapato hayo ya mabango.

“TBL wana mpango wa kuondokana na changamoto ya gharama kubwa ndio maana wakaona kuna umuhimu wa kuondoka kwenye kodi ya mabango kwa gharama zake zimekuwa kubwa sana ikiwemo pia kuanza kuzalisha umeme jua utakaoendesha uzalishaji na hivyo kuondokana na umeme usio na uhakika unaokatika kila mara”

About Alex

Check Also

maxresdefault

HOTELI YA KWANZA ARUSHA YATENGA MILIONI KUMI KWA AJILI YA YATIMA

UONGOZI wa hoteli ya kitalii ya New Safari Hoteli ya jijini Arusha umefanikiwa kujiwekea utaratibu …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

7 + 15 =