Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / WAZIRI HASUNGA NA MHANDISI METHEW MTIGUMWE, WARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA OFISI ZA WIZARA YA KILIMO

WAZIRI HASUNGA NA MHANDISI METHEW MTIGUMWE, WARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA OFISI ZA WIZARA YA KILIMO

Jengo la Wizara ya Kilimo likiwa katika hatua za mwisho kukamilika katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma. (Picha Zote Na Mathias Canal, Wizara ya Kilimo)
Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakikagua ujenzi wa Ofisi za Wizara unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
 Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakikagua ujenzi wa Ofisi za Wizara unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.

 

Waziri wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe wakiwa katika picha ya pamoja na mafundi wa Ofisi za Wizara katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Na
Mathias Canal, Wizara ya Kilimo-Dodoma
Waziri
wa Kilimo Mhe Japhet Hasunga (Mb) pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo
Mhandisi Methew Mtigumwe kwa kauli moja wameridhishwa na ujenzi wa Ofisi za
Wizara unaendelea kujengwa katika mji wa serikali Ihumwa Jijini Dodoma.
Mhe
Hasunga amesema kuwa Ofisi hizo zimekamilika kwa asilimia nyingi hivyo wakati
wowote kuanzia hivi sasa watumishi wa Wizara hiyo watapaswa kuhamia.
Ametoa
kauli hiyo mara baada ya kutembelea na kukagua hatua zilizofikiwa za ujenzi wa
Ofisi hizo leo Tarehe 14 Machi 2019.
Pamoja
na mambo mengine Waziri Hasunga alimpongeza Rais wa Tanzania Mhe Dkt John pombe
Magufuli kwa uamuzi wake ambao umetoa muelekeo wa serikali kuwa na mji wake
maalumu jambo hilo litaongeza ufanisi katika kuwahudumia wananchi.
Alisema
kuwa awali maamuzi ya Rais yalipotolewa wengi hawakuelewa makusudi ya ujenzi wa
mji wa kiserikali lakini pindi watumishi wa wizara mbalimbali watakapohamia
katika eneo hilo watabaini umuhimu wake.
Wakati
huo huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew Mtigumwe alimueleza
Waziri wa Kilimo kuwa ujenzi huo umefikia katika hatua za mwisho hivyo siku
chache zijazo maandalizi ya kuhamia Ihumwa yatakamilika.
Aliwapongeza
mafundi wanaoendelea na ujenzi huo kwa kuwa waaminifu na kukamilisha ujenzi wa
majengo hayo kwa wakati muafaka.
Serikali
kuhamia Dodoma ni sehemu ya kukamilisha safari iliyoanza miaka 42 iliyopita ya
kuhamishia makao makuu ya Serikali mkoani Dodoma.
MWISHO

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

18 − 5 =