Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / DC JOKATE AFUNGUA MAFUNZO WEZESHI YA ELIMU KWA WALIMU 408 WA KISARAWE KATIKA MUENDELEZO WA TOKOMEZA ZERO WILAYANI KWAKE AKISHIRIKIANA NA BRITISH COUNCIL

DC JOKATE AFUNGUA MAFUNZO WEZESHI YA ELIMU KWA WALIMU 408 WA KISARAWE KATIKA MUENDELEZO WA TOKOMEZA ZERO WILAYANI KWAKE AKISHIRIKIANA NA BRITISH COUNCIL

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akikata utepe jijini Dar es Salaam jana, kufungua mafunzo ya uwezeshaji kwa walimu wakuu 155 na walimu wa kawaida 253 kutoka wilayani Kisarawe leo,katika muendelezo wa kampeni yake ya Tokomeza Zero. Mafunzo hayo ya Siku Tatu Yaliyodhaminiwa na British Council Yanafanyika katika Chuo cha Duce na Kituo cha Elimu cha Mzimuni. Kushoto kwake ni Mkuu wa Miradi wa British Council,Atiya Sumar. Picha na Elisa Shunda
Mafunzo ya Uwezeshaji Yakiendelea katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam University College of Education (Duce)

 

Mkuu wa Miradi wa British Council,Atiya Sumar akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo.

 

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akipongezana na Mkuu wa Miradi wa British Council,Atiya Sumar (Kulia) baada ya kufungua mafunzo ya uwezeshaji kwa walimu wakuu 155 na walimu wa kawaida 253 kutoka wilayani Kisarawe leo,katika muendelezo wa kampeni yake ya Tokomeza Zero. jijini Dar es Salaam jana.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akiteta jambo na Mkuu wa Miradi wa British Council,Atiya Sumar (kulia) katika shughuli hiyo.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa chuo cha duce na Kituo cha Elimu cha Mzimuni Magomeni na Walimu.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya British Council na Viongozi wa chuo cha Duce.

………………………………………………………………………
NA:ELISA SHUNDA,DAR ES SALAAM
MKUU wa Wilaya ya Kisarawe,Jokate Mwegelo amefungua
mafunzo ya uongozi na uwezeshi wa maalifa na ujuzi wa kufundisha wanafunzi kwa
maafisa elimu wilaya na kata pamoja na walimu wakuu 155 na walimu wa kawaida
253 ambao walikuwa wakipatiwa mafunzo hayo katika eneo la chuo kishiriki cha
Dar es Salaam College of Education (Duce) na Kituo cha Elimu cha Mzimuni kwa
udhamini wa Taasisi Isiyo ya Kiserikali ya British Council jijini Dar es Salaam
leo.
Akizungumza wakati wa ufunguzi DC Jokate alisema kuwa
Taasisi ya British Council kwa kushirikiana na Chuo cha Duce na Kituo cha Elimu
cha Mzimuni kwa umoja wao wameona umuhimu wa kampeni yake ya Tokomeza Zero
wilayani Kisarawe ndio maana wakaamua kwa umoja wao wamsapoti katika kuleta
matokeo chanya wilayani Kisarawe na kuwashukuru kwa kutoa semina wezeshi
itakayowasaidia walimu hao kupata maalifa,ujuzi na mbinu mpya za ufundishaji
kwa wanafunzi.
“Nazishukuru taasisi ya British Council wakishirikiana na
Chuo cha Duce na Kituo cha Mzimu kwa kuweza kutusaidia sie viongozi wa wilaya
ya Kisarawe katika kuleta matokeo chanya kwa kuwapatia walimu wetu mbinu mpya
za ufundishaji wa kisasa zaidi hasa ukizingatia katika karne hii ya 21 mambo
mengi yamebadilika yamekuwa ya kisasa zaidi bila mwanafunzi kupata mwalimu
mwenye ujuzi wa kutosha hatoweza kuwa sawa na wanafunzi wenzake waliofundishwa
na walimu wenye ujuzi,maalifa na mbinu za kisasa,atatupwa mbali katika jambo
lolote lile” Alisema DC Jokate.
Pia DC Jokate aliongeza kwa kusema ili Mwanafunzi aendane
na ushindani kwa wenzake ni lazima apewe mbinu na uwezo wa Kuongea,uwezo wa
Kuwasiliana na uwezo wa Kufikilia (Critical Thinking) lengo ni kuwafanya
wanafunzi wa wilaya ya Kisarawe kuwa na uwezo wa hali ya juu ya kupambana na
changamoto yoyote watakayokutana nayo katika majukumu yao baada ya kumaliza
shule iwe ndani ya wilaya au nje ya Kisarawe.
Akizungumza kwa niaba ya Taasisi ya British
Council,Meneja Mradi wa taasisi hiyo,Ephrahim Kapungu alisema kuwa lengo la
British Council katika kuandaa mafunzo hayo ni kuwaongezea walimu wakuu uwezo
katika uongozi wa shule wanazoziongoza katika usimamizi mzuri wa kiutawala na
walimu wa kawaida kuwaongezea uwezo wa ujuzi,maalifa na mbinu mbalimbali za
ufundishaji ili wanafunzi wafaulu mitihani yao lakini pia kuwapatia elimu
itakayowasaidia kujiajiri wenyewe na kuendesha maisha yao.
“Sisi British Council tunashirikiana vizuri na wizara ya
elimu katika kuleta matokeo chanya lakini pia tunaahidi kushirikiana kwa
ukaribu na wilaya ya Kisarawe kutokana na muitikio mzuri ulioneshwa na Mkuu wa
Wilaya hiyo, Jokate Mwegelo lakini pia katika mpango mkubwa tunapenda kutoa nguvu
kwa Rais Wetu Dk.John Pombe Joseph Magufuli katika sera ya viwanda kama
unavyofahamu vijana wetu ndio walengwa wakubwa watakaofanya kazi kwenye viwanda
hivyo basi sie British tutajitahidi kuwapatia vijana wetu mbinu bora za
ufanyaji kazi za ushindani katika viwanda hivyo” Alisema Kapungu.
Akizungumza kwa Niaba ya Walimu,Kaimu Afisa Elimu Shule
za Msingi Wilaya ya Kisarawe,Madina Mussa, alisema kuwa mafunzo hayo yamewapa
uelewa mpya,mbinu mpya zitakazoweza kuondoa matokeo mabaya katika wilaya ya
Kisarawe pamoja na kupandisha ufaulu na kuondoa alama E katika shule za msingi
wilayani humo pamoja na kuifikia dira ya nchi ya kuwa na Mtanzania aliyeelimika
ifikapo mwaka 2025.

About bukuku

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

2 × one =