Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / TAA WAJIDHATITI NA UENDESHAJI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA

TAA WAJIDHATITI NA UENDESHAJI WA JENGO LA TATU LA ABIRIA

????????????????????????????????????

Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayesimamia Sekta ya  Ujenzi, Elias Kwandikwa (kulia), akifafanua jambo kwa Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege kutoka Wizarani, Eng. Emmanuel Raphael, wakati Kamati Kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipofanva ziara katika jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar Es Salaam.

????????????????????????????????????

Kaimu Kiongozi wa timu ya Wataalam (TECU), Mhandisi Barton Komba, akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, kuhusu hatua ya maendeleo ya mradi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) wakati walipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya jengo hilo, jijini Dar es Salaam.

????????????????????????????????????

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Mhe. Selemani Kakoso akitoa maelekezo kwa viongozi wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA), wakati kamati hiyo ilipofanya ziara kwenye Mamlaka hiyo ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa rada. Kushoto ni Naibu Waziri (Sekta ya Ujenzi), Elias Kwandikwa na  Kulia ni Naibu Waziri (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Eng Atashasta Nditiye.

????????????????????????????????????

Meneja mradi wa rada, Mhandisi Kriston Mwala, akitoa maelezo kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu ya maendeleo ya ujenzi wa rada mpya katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNIA) wakati kamati hiyo ilipokagua maendeleo ya ujenzi wake, jijini Dar es Salaam.

????????????????????????????????????

Muonekano wa rada mpya inayojengwa katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), ikiwa katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Rada hiyo ni moja kati ya rada nne mpya ambazo zinajengwa nchini.

………………………

Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), imebainisha kwamba itakua tayari kwa ajili ya utoaji wa huduma za uendeshaji katika Jengo la tatu la abiria pale mradi wa Ujenzi utakapokuwa umekamilika.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Bw. Paul Rwegasha alipokua akitoa taarifa fupi ya TAA kwa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Miundombinu ilipofanya ziara katika eneo la ujenzi huo.

Bw. Rwegasha amesema hatua mbalimbali za Maandalizi tayari zimeshachukuliwa kwa kushirikiana na wadau wa huduma hizo, ikiwa ni pamoja na utoaji wa mafunzo yanayohitajika kwa watendaji wa ngazi mbalimbali.

“Mamlaka inaendelea kufanya taratibu za maandalizi ya utoaji huduma za uendeshaji katika Jengo la tatu la abiria, katika mpango huo tayari mafunzo kwa watendaji mbalimbali yameanza na hivi sasa watendaji 40 wapo Korea ya Kusini katika mafunzo”, amesema Bw. Rwegasha.

Aidha Bw. Rwegasha amebainisha kwamba katika utekelezaji mpango wa uhamishaji shughuli, Mamlaka imejipanga kuhakikisha hakuna madhara yeyote ya kiuendeshaji yanajitokeza.

“Mamlaka itahakikisha kwamba inazuia athari zote zinazoweza kutokana na zoezi la uhamishaji wa shughuli za uendeshaji ikiwa ni pamoja na kuchelewa kwa ndege na abiria, uharibifu wa mitambo, madhara ya kiusalama na kadhalika”, amefafanua Bw. Rwegasha.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Idara ya Viwanja vya Ndege kutoka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Emmanuel Raphael, amebainisha kwamba hadi kufika mwezi February 2019 utekelezaji wa kazi zote ulifikia asilimia 95.

“Ujenzi wa kazi zote za Ujenzi umefikia 95%, ambapo mchanganuo unaonesha kwamba ujenzi wa jengo umefikia 96%, maegesho ya magari 92%, maegesho ya ndege 98% na kwa ujumla kazi zinaenda vizuri na zinatarajiwa kukamilika Mwezi Mei 31, 2019”, alisema Mhandisi Raphael.

Naye, Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Uchukuzi na Mawasiliano), Mhandisi Atashasta Nditiye, amebainisha kwamba mpaka sasa Wananchi wa Kipawa waliopisha upanuzi wa kiwanja wameshalipwa fidia na kwamba mpaka sasa hamna mgogoro wa fidia.

Akitoa majumuisho baada ya ziara ya kamati katika eneo la ujenzi, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Mhe. Moshi Seleman Kakoso, amesema kwa ujumla kamati imeridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa na kwamba wameridhishwa na namna fedha ya Serikali ilivyotumika.

“Kwa ujumla kamati imeridhishwa na hatua ya ujenzi iliyofikiwa, thamani ya fedha inaonekana, lakini natoa wito kwa TAA kuongeza kasi ya maandalizi ili kwenda sawa na kasi ya ujezi huu, lakini pia mjipange kuongeza wafanyakazi ili kuhakikisha kwamba watendaji wa huduma za uendeshaji wanajitosheleza”, amesema Mhe. Kakoso. 

Katika hatua nyingine, kamati hiyo ilifanya ziara katika Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA),  na  kuridhishwa na hatua za mwisho za ujenzi wa rada mpya iliyojengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere(JNIA) na kusisitiza kuitunza rada hiyo kwani kutaiwezesha katika utaoji huduma bora wa kuongoza ndege na kulifanya anga la Tanzania kuwa salama.

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

two × one =