Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / UTEPE MWEUPE SULUHISHO LA VIFO VYA MAMA NA MTOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA .

UTEPE MWEUPE SULUHISHO LA VIFO VYA MAMA NA MTOTO WAKATI WA KUJIFUNGUA .

yu1

Meneja mahusiano kutoka shirika la utepe mweupe Anna kushoto akitoa maelezo juu ya kazi wanazozifanya katika kupambana na vifo vitokanavyo na uazazi

yu2

Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro kwa Niaba ya Waziri Ummy Mwalimu akizindua mpango wa utepe mweupe katika maadhimisho yaliyofanyika Manispaa ya Bukoba.

yu3

Mgeni rasmi Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawiro Mkuu wa Wikaya ya Bukoba akionesha mpango wa utepe mweupe Mara baada ya kuzindua

yu4

Baadhi ya wadau wa sekta ya afya wakishiriki katika maandamano hayo.

yu5

Waenesha bodaboda wakishiriki katika maandamano hayo kuelekea viwanja vya Gymkana mjini Bukoba

yu6

Pichani ni sehemu ya waandamanaji na wadau wa sekta ya Afya, wakitembea kwa maandamano wakikatiza maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Bukoba kuelekea viwanja vya Gymkhana.

………………………………………………………………………..

Abdullatif Yunus, Bukoba – Kagera.

Maadhimisho ya siku ya Muungano wa utepe mweupe na uzazi salama katika Mkoa wa Kagera yamefanyika Kitaifa Mkoani Kagera Machi 15, 2019 huku jamii ikihimizwa kuacha ukatiri wa kijinsia kwa wanawake na wasichana.

Awali Maadhimisho hayo yalitanguliwa na mandamano ya wananchi mamia kwa maelfu na kisha kilele chake Kufanyika katika viwanja ya Gymkana katika manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera yakiwa na kauli mbiu “komesha unyanyasaji kwa wanawake na wasichana,okoa maisha wakati wa uzazi”.

Meneja Mawasiliano kutoka muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama Anna Sawaki amesema maadhimisho hayo kuwa yana lengo la kupunguza vifo kwa wananwake wakati wa kujifungua. Na kuongeza
kuwa takwimu zinaonesha vifo vitokanavyo na uzazi vinaongezeka badala ya kupungua kutokana na unyanyasaji wanaoupata akina mama pindi wawapo wajawazito na wakati wa kujifungua.

Kwaupande wake Rose Mlayi ambaye ni mratibu wa Taifa wa muungano wa utepe mweupe wa uzazi salama ameiomba jamii kukomesha ukatili kwa wanawake na wasichana, ili kuokoa maisha yao wakati wa uzazi.
Bi Rose amesema kuwa upungufu wa vituo vya afya na zahanati katika maeneo mengi ni moja ya vyanzo vinavyosababisha vifo kwa akina mama wengi wakati wa kuelekea kujifungua hasa maeneo ya vijijini kutokana na wamama hao kutembea mwendo mrefu pamoja na baadhi ya mira potofu kutoka kwa jamii ya kuwazuia wanawake kujifungulia katika vituo vya afya.

Katika hotuba ya Waziri wa afya,maeneleo ya jamii jinsia wazee na watoto Ummy Mwalimu iliyosomwa kwa niaba yake na Mkuu wa wilaya ya Bukoba Deodatus Kinawilo,amesisitiza kuwa Serikali kupitia idara zake inaendelea kukomesha vitendo hivyo, ikiwemo kuendelea na mikakati yake ya kutokomeza vifo vitakavya na uzazi pingamizi.
Waziri ummy ameongeza kuwa wizara yake inaendelea kuboresha sekta ya afya hasa upande wa vituo vya afya pamoja na vifaa tiba ambapo pia ameeleza mkakati wa kuanzisha vituo vya huduma jumuishi kwa kila kituo cha afya.

About bukuku

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

nineteen − 7 =