Saturday , March 23 2019

Home / MCHANGANYIKO / VYOMBO VYA UMMA VYATAKIWA KUSIMAMIA HAKI YA UPATIKANAJI TAARIFA

VYOMBO VYA UMMA VYATAKIWA KUSIMAMIA HAKI YA UPATIKANAJI TAARIFA

Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika ,tawi la Tanzania (Misa-Tan) Salome Kitomary akiongea jambo wakati wa Mafunzo kwa watumishi wa Mahakama mkoa wa Kilimanjaro .

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika ,tawi la Tanzania (Misa-Tan) Salome Kitomary akisikiliza mawazo mbalimbali kutoka kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Mkufunzi katika Mafunzo yanayowahusisha watumishi wa Mahakama,Wakili James Marenga akiwasilisha mada katika mafunzo hayo yanayofanyika Hoteli ya Leopard mjini Moshi.
Baadhi ya Washiriki katika mafunzo hayo wakifurahia jambo wakati wakifuatilia mada zilizokuwa zikitolewa na wakufunzi.

Normal
0

false
false
false

EN-US
X-NONE
X-NONE

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

VYOMBO  vya umma vimetakiwa
kuwasimamia haki ya upatikanaji wa taarifa ikwa ni pamoja na kuwa wakala kwa mwananchi
yoyote atakayehitaji kupata haki isipokuwa kama kuna sheria inayotoa ufafanuzi
wa msingi kwanini zisitolewe.
Hayo yamelezwa na Mkufunzi katika mafunzo kwa watumishi wa
Mahakama yanayofanyika katika Hoteli ya Leopard mjini Moshi,Wakili James
Marenga wakati akiwasilisha mada iliyohusu Muktadha wa Kisheria kwenye haki ya
kupata taarifa.
Alisema haki ya kupata habari  inapatikana kwenye mikataba ya kimataifa
ambayo ndimo misingi ya uhuru wa kujielezea imejengeka na kwamba ni tamko la
kimataifa la haki za binadamu la mwaka 1948.
“Ibara ya 19  ya Tamko
hilo inasema kuwa  Kila mmoja ana haki
ya uhuru wa kutoa na kueleza maoni yake; haki hii inahusu pia uhuru wa
kutoa  maoni yake bila kuingiliwa kati,
na uhuru wa kutafuta na kutoa taarifa na maoni kwa njia yoyote bila kujali
mipaka
.” Alisema Marenga.
Alisema katika tamko la Afrika juu ya miiko na kanuni  za watumishi wa umma na utawala limeelekeza
kuwa  Utumishi wa Umma na Utawala
utahakikisha kuwepo na taarifa na utaratibu wa namna ambavyo utumishi wa umma
unavyotakiwa kutoa huduma.
Marenga alisema utumishi wa umma na utawala wanatakiwa kutoa
taarifa kwa wananchi juu ya mambo yanayowahusu na kama kuna maamuzi juu yao
yametolewa katika misingi gani na kwa sababu gani na kama kuna namna yoyote ya
kukata rufaa juu ya maamuzi hayo. 
“ Utumishi wa Umma na Utawala  uweke mfumo wa mawasiliano  na mchakato
wa kujulisha umma juu ya huduma wanazozitoa  ili kuwezesha upatikanaji wa taarifa  kwa watumiaji na kupata mrejesho kutoka kwao.
Mapema washiriki wa mafunzo hayo ya siku tatu wameeleza
kupata mwanga zaidi kutokana na mfunzo hayo hasa katika maeneo ya utoaji huduma
kwa wananchi bila kujali hali za wahusika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa
kufuata taratibu zilizoelekezwa kwa mujibu wa Sheria ya upatikanaji  taarifa.
“moja ya mambo tunayojifunza ni pamoja na kuacha changamoto
za nyumbani mara baada ya kuingia katika maeneo yetu ya kazi ,na hii husaidia
ufanisi katika kumuhudumia mwananchi ambaye ni mteja wetu “alisema Massawe
mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo.
Mafunzo hayo yanayoendeshwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari
Kusini mwa Afrika –Misa Tan kwa kushirikiana na taasisi ya kijerumani ya
Friedrich Ebert Stiftung  yamelenga  kuwakumbusha watumishi hao wa Mahakam juu
upatikanaji wa taarifa na maadili kwa utumishi wa umma pamoja na utoaji huduma
kwa wateja.
Mwisho.

About Alex

Check Also

WAKITAZAMA

Waziri Biteko Asema Wizara Iko Tayari kuwahudumia Watanzania kutokea Ihumwa

Muonekano wa Jengo la Wizara ya Madini linalojengwa katika Mji wa Serikali eneo la Ihumwa.  …

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

three × 1 =